MWANZA: KESI YA MAAMUZI YA KUPINGA MATOKEO JIMBO LA TARIME VIJIJINI YAHAILISHWA LEO.
Mahakama
Kuu Kanda ya Mwanza leo imeahirisha Kesi ya Kupinga Matokeo ya Uchaguzi
Mkuu Jimbo la Tarime Vijijini uliofanyika Novemba 25,2015. Kesi hiyo
ilifunguliwa aliekuwa Mgombea wa Jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi
CCM Christopher Ryoba Kangoye akiiomba Mahakama kutengua Ushindi wa
Mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema John Heche
aliechaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo hilo kwa kuwa uchaguzi huo haukuwa wa
huru na haki.
Na:George Binagi.
Kesi
hiyo ambayo ilianza kusikilizwa January 19,2015 chini ya Jaji wa
Mahakama hiyo Mhe.Lameck Mlacha leo imeahirishwa hadi kesho January
28,2015 majira ya saa nane mchana itakapotolewa maamuzi yake.
Mjibu
maombi katika kesi hiyo (John Heche) anawakilishwa na Mawakili Tundu
Lisu (leo hakuwa Mahakamani) pamoja na Paul Kipeja (alikuwepo
Mahakamani).
Baada
ya Kesi hiyo Kuahirishwa, Katibu wa Chadema Mkoani Mara Mwl.Chacha
Heche (Pichani Juu anaehojiwa) ameiomba Mahakama kutoa maamuzi ya Kesi
hiyo ili kuwapunguzia gharama kwa kuwa ambazo zinajitokeza wakiwa Jijini
Mwanza kufuatilia maamuzi ya kesi hiyo.
Barnabas
Nyangi Lubare ambae ni mmoja wa Wakazi wa Jimbo la Tarime akihojiwa na
Wanahabari baada ya kesi kuahirishwa amesema kuwa wanatarime vijijini
wana imani na Mahakama na kwamba kesi hiyo ni sehemu ya changamoto kwa
mbunge wao na kwamba wembe ni ule ule wa kushinda kuanzia jimboni hadi
Mahakamani.
Barnabas Nyangi Lubare ambae ni mmoja wa Wakazi wa Jimbo la Tarime akihojiwa na Wanahabari baada ya kesi kuahirishwa.
Paul
Kipeja ambae ni Wakili upande wa Mjibu Maoni akizungumza na wanahabari
baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kuahirisha kutoa Maamuzi ya kesi
ya Kupinga Matokeo Jimbo la Tarime Vijijini.
Anasema
kama ilivyokuwa katika Kesi ya Kupinga Matokeo ya Uchaguzi Jimbo la
Bunda Mjini iliyofunguliwa na Wapiga kura wa Jimbo hilo dhidi ya Esther
Bulaya (Mbunge), ndivyo itakavyokuwa hata katika Jimbo la Tarime
Vijijini kwa maana ya mteja wao (John Heche) kushinda kesi inayomkabiri.
No comments:
Post a Comment