SHIRIKA LA WORLD LUNG FOUNDATION(WLF) LATOA MSAADA WA VIFAA VYA KUMSAIDIA MAMA MJAMZITO KUJIFUNGUA(VACUUM EXTRACTORTS) KWA HOSPITAL YA MKOA YA KIGOMA.
Mkurugenzi
mkuu wa World Lung Foundation(WLF) Dk Nguke Mwakatundu akimkabidhi
Katibu tawala wa Mkoa wa Kigoma Mhandisi John Ndunguru moja ya kifaa
cha kumsaidia mama mjamzito kuvuta mtoto wakati wa kujifungua.
Katibu
tawala wa Mkoa wa Kigoma John Ndunguru akikabidhi moja ya kifaa cha
kumsaidia mama mjamzito kujifungua salama kwa kumvuta mtoto kwa uongozi
wa hospita ya Mkoa, uliotolewa na shirika la World Lung Foundation.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Kigoma John Ndunguru akiongea na waandishi wa habari
baada ya kukabidhi msaada wa vifaa saba vya kumsaidia mama mjazito
kujifungua katika hospital ya Mkoa wa Kigoma msaada uliotolewa na
shirika la Word Lung Foundation
SHIRIKA
LA WORLD LUNG FOUNDATION(WLF) LATOA MSAADA WA VIFAA VYA KUMSAIDIA MAMA
MJAMZITO KUJIFUNGUA (VACUUM EXTRACTORTS) KWA HOSPITAL YA MKOA YA
KIGOMA.
Na Editha Karlo wa blog ya jamii, Kigoma
Shirika
lisilo la kiserekali la Word Lung Foundation(WLF) limetoa msaada wa
vifaa saba kwaajili ya kumsaidia mama mjamzito wakati akijifungua
kumvuta mtoto aliyeshindwa kutoka kwa kutumia ombwe(vacuum extractors)
vifaa hizo vimetolewa katika hospital ya Mkoa wa Kigoma.
Akiongea
wakati wa kukabidhi msaada huo wa vifaa vya kusaidia akina mama
wajawazito kujifungua salama kwa uongozi Serekali ya Mkoa na hospital
Mkurugenzi Mkuu wa wa shirika hilo Dk Nguke Mwakatundu alisema Kuwa
shirika hilo limekuwa mstari wa mbele kuhakikisha vifo vya akina mama na
watoto wachanga vinapungua.
Alisema
utumiaji wa vifaa hivyo vya kuvuta watoto inasaidia akina wengi
kujifungua bila ya upasuaji jambo linalowapunguzia adha mbalimbali
zitokanazo na upasuaji kama vile maumivu, kuuguza kidonda muda mrefu
pamoja na matatizo mengine.
Alisema
vifaa hivyo vinathamani ya shilingi 30,450,000 ambavyo vitaboresha
utoaji wa huduma kwa akina mama wakati wa kujifungua.
Naye
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Kanali mstaafu
Issa Machibya alisema kuwa uongozi wa Mkoa wa Kigoma unalishuru shirika
hilo kwa juhudi wanazofanya za kupunguza vifo vya akina mama wajawazito
na watoto wachanga katika Mkoa wa Kigoma.
"Kwakweli
World Lung Kigoma mnaipenda sana kwani ipo Mikoa mingi hapa nchini
yenye matatizo haya lakini nyie mmechagua kuja kufanya kazi kwenye mkoa
huu nawapongeza kwa hili"alisema Katibu tawala wa Mkoa
Alisema
Mkoa utashirikiana shirika hilo katika kuhakikisha vifo vya akina mama
wajawazito na watoto wachanga vinapungua Mkoani Kigoma.
Naye
Kaimu Mganga Mkuu wa hospital ya Mkoa wa Kigoma maweni Dk Fadhil Kabaya
alisema kuwa kwa kipindi cha mwaka mmoja shirika hilo limeweza
kushirikiana na vituo vya afya 9 wanavyofanya navyo kazi na kupata
mafanikio mbalimbali.
"Akina
mama 18281 walijifungulia katika vituo hivyo, akina mama 1613
walifanyiwa upasuaji na akina mama 166 walipatiwa huduma ya kumvuta
mtoto kwa kutumia ombwe yaani vacuum extraction, pia vifo vinavyotokana
na uzazi vimepungua kutoka 49 mwaka 2014 hadi vifo 38 mwaka 2015 sawa
na asilimia 22"alisema Dk Fadhil
No comments:
Post a Comment