MKUU WA WILAYA YA RUANGWA MKOA WA LINDI,MARIAM MTINA ATOA MACHOZI WAKATI WA KUPOKEA MSAADA MASHINE TOKA VODACOM FOUNDATION
Mkuu
wa Wilaya ya Ruangwa Mkoa wa Lindi,Mariam Mtina(wasita toka
kushoto)akimsikiliza kwa umakini Muuguzi Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya
hiyo, Omary Rajabu(kulia)alipokuwa akiwaelezea baadhi ya wafanyakazi wa
Vodacom Tanzania,Wauguzi wa hospitali hiyo na wananchi jinsi mashine
inayofyonza uchafu(Electrical Suction machine) kwa watoto waliozaliwa
kabla ya wakati”Njiti” Zaidi ya shilingi Milioni 6/- zilitumika katika
kunua vifaa hivyo na kutolewa msaada na Vodacom Foundation kupitia
taasisi inayojishughulisha na watoto hao ya Doris Mollel.
Mkuu
wa Wilaya ya Ruangwa Mkoa wa Lindi,Mariam Mtina(wapili toka
kushoto)pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania, Wauguzi wa
hospitali hiyo na wananchi wakimsikiliza Mganga Mkuu wa Wilaya ya
Ruangwa,Dkt Japhet Simeo(kushoto)akiwaelimisha jinsi mashine ya Oxygen
inavyosaidia watoto waliozaliwa kabla ya wakati”Njiti” kupumua wakati wa
hafla fupi ya makabidhiano ya msaada wa mashine hizo zilizogharimu
zaidi ya shilingi milioni 6/- na kukabidhiwa na Vodacom Foundation
kupitia taasisi inayojishughulisha na watoto hao ya Doris Mollel.
Mkuu
wa Wilaya ya Ruangwa Mkoa wa Lindi,Mariam Mtina(katikati)akitoa
shukurani kwa niaba ya wananchi wake kwa Meneja wa Vodacom
Foundation,Sandra Oswald na Mwanzilishi wa taasisi ya Doris Mollel
inayojishughulisha kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya
wakati”Njiti”,Doris Mollel(kulia)kuhusiana na msaada wa mashine ya
kupumulia na vifaa mbalimbali uliotolewa na Vodacom Foundation kupitia
taasisi ya Doris Mollel vya kuwasaidia watoto hao wanaozaliwa katika
wilaya hiyo.Vifaaa hivyo viligharimu zaidi ya shilingi milioni 6/-
Mkuu
wa Wilaya ya Ruangwa Mkoa wa Lindi,Mariam Mtina(watatu toka
kushoto)akipokea msaada wa mashine inayofyonza uchafu kwa watoto
waliozaliwa kabla ya wakati”Njiti”kwa niaba ya wananchi wa wilaya hiyo
toka kwa Meneja wa Vodacom Foundation, Sandra Oswald.Msaada huo
uliotolewa na Vodacom Foundation kupitia taasisi ya Doris
Mollel,Uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 6/-
Baadhi
ya wakazi wa Wilaya ya Ruangwa Mkoa wa Lindi,wakifurahia msaada wa
mashine mbalimbali uliotolewa na Vodacom Foundation kupitia taasisi ya
Doris Mollel inayojishughulisha kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya
wakati”Njiti”Msaada huo ulikabidhiwa hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment