MBUNGE MWAMOTO ACHANGIA UJENZI WA DARASA LA CHEKECHEA , ASEMA RAIS DR MAGUFULI KAFUTA ADA NA MICHANGO SIO MICHANGO YA UJENZI WA SHULE
Mbunge
wa jimbo la Kilolo Bw Venance Mwamoto akikabidhi fedha akisi cha
Tsh 500,000 kati ya Tsh milioni 1 alizoahidi kuchangia ukarabati wa
darasa la chekechea kijiji cha Isele kata ya Ilula
........................................
Na MatukiodaimaBlog
MBUNGE
wa jimbo la Kilolo mkoani Iringa Bw Venance Mwamoto achangia kiasi
cha Tsh milioni 1 kwa ajili ya kuwaunga mkono wananchi wake kijiji
cha Isele kata ya Ilula wilaya ya Kilolo ambao wamejitolea kufanya
ukarabati wa darasa la chekechea kwa lengo la kusogeza elimu kwa
watoto kijijini hapo.
Huku
akiwataka wananchi wote kuendelea kuchangia ujenzi wa vyumba vya
madarasa ,shule na nyumba za walimu na kuwa serikali ya Rais Dr John
Magufuli imefuta ada na michango na sio uchangiaji wa ujenzi .
Akikabidhi
kiasi cha Tsh 500,000 kati ya Tsh milioni 1 ambayo amepanga
kuwachangia wananchi hao leo mbunge huyo alisema kuwa baada ya
kufika kuhamasisha wananchi kuchangia shughuli za kimaendeleo
zikiwemo za elimu alikutana na changamoto ya ukosefu wa darasa la
awali katika kijiji hicho na hivyo kuwahamasisha wananchi kuanza
kutatua tatizo hilo.
Bw
Mwamoto alisema kuwa baada ya kufika katika kijiji hicho
uongozi wa kijiji ulimtembeza eneo hilo ambalo wananchi walikusudia
kufanya ukarabati wa darasa kwa ajili ya wanafunzi wa chekechea na
kuwa mahitaji yote pamoja na nguvu za wananchi ilikuwa ni Tsh milioni
2 na hivyo kulazimika kuchukua mzigo wa kuchangia pesa kiasi hicho
cha Tsh milioni 1
"
Kimsingi hali ya darasa lile haikunifurahisha hivyo niliwataka
kufanya marekebisho ili watoto hao kuweza kusoma katika mazingira
bora zaidi na hii pesa nimetoa kwa ajili ya kuanza kazi hiyo na pindi
wakimaliza nitamalizia pesa iliyosalia "
Hata
hivyo mbunge Mwamoto aliwataka wananchi kuendelea kuchangia
shughuli za kimaendeleo hasa elimu na kuwa serikali ya Rais Dr John
Magufuli imefuta michango na ada kwa elimu ya msingi na sekondari na
sio kwamba imefuta michango ya ujenzi wa nyumba za walimu ama shule .
Hivyo
aliwataka wananchi kuendelea jitihada zao za kushiriki kuchangia
maendeleo ya elimu kwa maana ya ujenzi wakati serikali imechukua
jukumu la kuwalipia watoto hao ada na chakula kwa shule za sekondari
za bweni ambazo zipo chini ya serikali.
Alisema
kuwa yeye kama mbunge wao kamwe hata waacha yatima katika shughuli
yoyote ya kimaendeleo atahakikisha anashirikiana na wananchi hao
kikamilifu katika kuitekeleza .
Afisa
mtendaji wa kata ya Ilulu Bw Chusi Ashrafu akimpongeza mbunge Mwamoto
kwa kuunga mkono nguvu za wananchi hao alisema kuwa hadi sasa
mwitikio wa wananchi katika shughuli za kimaendeleo ikiwemo ya
umaliziaji wa madarasa hayo ni nzuri .
Alisema
hadi sasa wananchi wa vitongiji vyote vitatu wameonyesha
ushirikiano mzuri zaidi kwa kila kitongoji kuchangia kiasi cha Tsh
200,000 na wana jumla ya Tsh 600,000 kati ya Tsh milioni 1 ambayo
wananchi walipaswa kuchangia wakati mbunge akiahidi kuchangia Tsh
milioni 1 na kwa sasa mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilolo pia ameahidi
kumuunga mkono Mbunge Mwamoto kwa kuchangia Tsh 200,000 hivyo
wanamatumaini kasi ya ujenzi huo hadi sasa imefikia pazuri zaidi.
No comments:
Post a Comment