Zantel Tanzania yamtangaza Benoit Janin kuwa Mkurugenzi mpya
Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel leo imemtangaza bwana
Benoit Janin kuwa Mkurugenzi mpya wa kampuni hiyo.
Bwana
Janin anachukua nafasi ya Pratap Ghose ambaye ameiongoza kampuni hiyo kwa muda
wa miaka mitatu.
Uteuzi
wa Janin unafatia kampuni ya Millicom kununua hisa za kampuni ya Zantel ambapo
sasa itashirikiana na serikali ya Zanzibar kuhakikisha kampuni ya Zantel inakua
na inaboresha huduma zake.
Benoit,
ambaye ana uzoefu wa zaidi ya miaka 16 katika
sekta ya mawasiliano katika nchi za Afrika na masoko yanayokua, alikuwa
Mkurugenzi wa kampuni ya Tigo nchini Chad kwa muda wa miaka mitatu, ambapo
aliiwezesha kuwa kampuni namba moja nchini humo.
Kabla ya kujiunga na Millicom, Benoit amefanya kazi
na kampuni ya mawasiliano ya Vimpelcom kama Mkugenzi wa Biashara nchini
Cambodia, huku pia akiwa ameshikilia nafasi mbalimbali za kiuongozi katika
kampuni ya Orange.
Akizungumzia majukumu yake mapya, Benoit alisema
anatarajia kushirikiana na wafanyakazi wa Zantel katika kuhakikisha kampuni inakua
na kufikia malengo yake.‘Nina
furaha kubwa kujiunga na kampuni ya Zantel na ninatarajia kushirikiana na
wafanyakazi wenzangu kuongeza idadi ya wateja, pamoja na kusimamia ukuaji wa
kampuni kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato’ alisema Benoit.
Kama sehemu ya majukumu yake mapya, Bwana Janin ataboresha
huduma za mtandao za Zantel pamoja na kuzindua huduma za 4G hapo mwakani
No comments:
Post a Comment