Header Ads

Airtel yazindua mnara wa mawasiliano Mazinde wilaya ya Korogwe

Katika juhudu zake za kuhakikisha watanzania waishio mjini na vijiji wanapata huduma bora za mawasiliano , kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua mnara wa mawasiliano katika kata ya mazinde wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga.

Uzinduzi huo wa mnara wa mawasiliano utawahakikishia wakazi wa Mazinde na vijiji vya jirani mawasiliano ya uhakika katika kuendesha shughuli zao za kijamii na kiuchumi kila siku ikiwemo kilimo cha katani.

Akiongea wakati wa uzinduzi, Mkuu wa wilaya ya Korogwe, Hafsa Mtasiwa alisema" tunafurahi kuwa na mnara huu wa mawasiliano kwaajili ya wakazi wa wilaya ya mazinde ambao utasaidia kukuza biashara zao na kuinua utandawazi kupitia simu zao za mkononi".

Aliongeza kwa kusema" mawasiliano ndio chachu ya maendeleo ya uchumi wa jamii na ulimwengu kwa ujumla. na nimatumaini yetu kuwa huduma hii inayozinduliwa hapa leo itachangia kwa kiasi kikubwa endeshaji wa mashamba ya katani, kilimo, biashara mbalimbali na pia kuchagia katika kubadilisha maisha ya wengi na kwa hilo tunapenda kuwashukuru sana Airtel ".

Kwa upande wake, Meneja mauzo wa kanda ya kaskazini, Aluta kweka amesema kampuni yake iko mstari wa mbele katika kuhakikisha inatoa huduma za mawasiliano za uhakika zitakazorahisisha ukuaji wa uchumi na pato la taifa.

" katika ulimwengu wa leo wa sayansi na technologia watanzania wanatakiwa kuwezesha ili kupata fulsa zitokanazo na huduma bora za mawasiliano. Tunaamini mnara huu hautawahakikishia wakazi wa hapa mawasiliano ya uhakika tu bali utachangia kwa kiasi kikibwa katika kuongeza pato la taifa kwa ujumla".

Kufatia uzinduzi huo, zaidi ya wakazi takribani 10,000 na vijiji vitatu vitafaidika na bidhaa na huduma mbalimbali ikiwemo , huduma za intaneti, Airtel money, yatosha na nyingine nyingi
Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Hafsa Mtasiwa (wa pili kulia)) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mnara wa kampuni ya simu za mkononi Airtel Kata ya Mazinde wilaya ya Korogwe mkoani Tanga. anayeshuhudia kushoto ni Meneja wa Kampuni ya Simu ya Airtel Kanda ya Kaskazini Aluta Kweka.

No comments:

Powered by Blogger.