Header Ads

Katibu Mkuu wa Uchukuzi atembelea eneo inapojengwa Reli Mpya ya kisasa ya standard gauge

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka,akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu Rwanda, Rwakunda Christian,wakati walipotembelea ujenzi wa reli mpya ya kisasa, iliyoanza kujengwa Mkoani Pwani, katika eneo la Soga.
 Muonekano wa ujenzi wa reli mpya wa kisasa Standard Gauge, ambayo inaendelea kujengwa katika eneo la soga mkoani Pwani.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka (wa tatu kutoka kulia), akiwa katika picha pamoja na Uongozi wa Taasisi inayosimamia usafirishaji katika Ukanda wa Kati pamoja na Viongozi wa Nchi zinazotumia ukanda wa Kati, wakati walipotembelea ujenzi huo hivi karibuni, katika eneo la Soga, Pwani.
Muonekano wa Vituo vya Reli hiyo Mpya ya kisasa ya standard Gauge, itakapokamilika.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu Rwanda, Rwakunda Christian, akiteta jambo na maafisa kutoka nchi zinazotumia ukanda wa kati kusafirisha bidhaa zao, wakati wakiangalia ramani ya reli mpya ya kisasa, walipotembelea ujenzi wa reli mpya ya kisasa ya standard gauge, hivi karibuni Mkoani Pwani. Viongozi hao walifurahishwa na maendeleo ya ujenzi huo kwa sababu utarahisisha usafirishaji wa mizigo kwani itapitisha mzigo zaidi na ukubwa wa reli hiyo utaongeza spidi ya treni.(Habari Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)

No comments:

Powered by Blogger.