Header Ads

UPDATES KUTOKA DODOMA: RAIS KIKWETE AFUNGA MKUTANO MKUU WA CCM MJINI DODOMA LEO, KUMTAMBULISHA MAGUFULI UWANJA WA JAMHURI JANA

 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama, wakati wa kuufunga Mkutano huo jioni hii kwenye Ukumbi wa Mikutano wa CCM (Dodoma Conveition Centre), uliopo Mjini Dodoma. CCM wanafanya mkutano mkubwa wa kumtambulisha Mgombea wao jioni hii kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwatambulisha Mgombea Urais wa  CCM, Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mgombea Mwenza, Mh. Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuufunga Mkutano huo.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin Mkapa akimkumbatia Dkt. John Pombe Magufuli wakati akimpongeza kwa ushindi alioupata.
Mgombea Urais wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Mzee Pius Msekwa na Mzee Ali Hassan Mwinyi.

No comments:

Powered by Blogger.