Ofisi ya Kambi ya Upinzani Bungeni yaandaa futari wakati wa kikao cha ukawa jijini Dar es salaam
Katibu
Mkuu wa CHADEMA Dkt. Willibroad Slaa akishiriki futari iliyoandaliwa na
Ofisi ya Kambi ya Upinzani Bungeni wakati wa kikao cha Viongozi Wakuu
wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na wabunge wa umoja huo
kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam kujadili mikakati mbalimbali ya
ushindi kuelekea uchaguzi mkuu. Kushoto kwake ni Mbunge wa CUF, Ali
Khamis Seif (Mkoani) na kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa NLD
Zanzibar, Ahmad Hemed.
Mwenyekiti
wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe akijadiliana jambo na Makamu Mwenyekiti
wa chama hicho Zanzibar, Said Issa Mohamed (katikati) pamoja na Mbunge
wa Bunge la Afrika Mashariki Ndelakindo Kessy (kushoto) huku wakishiriki
futari iliyoandaliwa na Ofisi ya Kiongozi wa Upinzani Bungeni wakati wa
kikao cha Viongozi Wakuu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na
wabunge wa vyama vinavyounda umoja huo kilichofanyika jana jijini Dar es
Salaam kujadili mikakati mbalimbali ya ushindi kuelekea uchaguzi mkuu.
Baadhi
ya Wabunge wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kutoka kushoto, Naomi
Kaihula (Viti Maalum CHADEMA), Salum Baruan (CUF- Lindi Mjini) na
Mohamed Habib Mnyaa wakishiriki futari iliyoandaliwa jana jijini Dar es
Salaam na Ofisi ya Kambi ya Upinzani Bungeni, wakati wabunge wa vyama
vinavyounda umoja huo waliposhiriki kikao cha Viongozi Wakuu wa UKAWA
(Summit) kilichojadili mikakati mbalimbali ya maandalizi ya ushindi
kuelekea uchaguzi mkuu.
Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar Said
Issa Mohamed akijiandaa kuwamiminia uji baadhi ya wabunge wa vyama
vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wakati wa kula futari.
Wabunge hao walikuwa wakihudhuria kikao cha Viongozi Wakuu wa UKAWA
kilichofanyika juzi jijini Dar es Salaam kujadili mikakati mbalimbali ya
ushindi kuelekea uchaguzi mkuu. Walioketi kutoka kushoto ni Seleman
Bungala Bwege (CUF- Kilwa Kusini),Mohamed Habib Mnyaa (CUF-Mkanyageni)
na Mama Riziki.
Wabunge wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wakati wa kula futari.
No comments:
Post a Comment