Umoja wa Ulaya, UN; Tutapigania Uhuru wa Habari Siku Zote
Na Joachim Mushi, Morogoro
UMOJA
wa Nchi za Ulaya nchini Tanzania (EU) umepinga vikali vitendo vya
kikatili na unyanyasaji wameokuwa wakifanyiwa na vyombo vya dola vya
Serikali wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao ambapo ilitokea
mwanahabari mmoja kuuwawa. Alisema hawatachoka kukemea matukio hayo ya
unyanyasaji kwani yanafifisha uhuru wa habari.
Akizungumza
leo mjini Morogoro katika Maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
Duniani, Kiongozi Mkuu wa Mabalozi hao, Balozi Filiberto Cerianse
Bregondi alisema EU itaendelea kupinga namna yoyote ya unyanyasaji kwa
wanahabari makundi yote wakiwemo wa mitandao ya kijamii hadi utakapo
kuwepo uhuru kamili wa vyombo vya habari.
"...Tulifanya hivyo kwa mauaji yalipotokea na tutaendelea kufanya hivyo
siku zote watakapo kamatwa na kupigwa wakiwa kazini...Tunajua huenda
haitoshi lakini hii ni kutokana na tofauti mbalimbali za kiutendaji,"
alisema Balozi Cerianse Bregondi.
Alisema
kupinga unyanyasaji kwa wanahabari haina maana wanachoandika wanahabari
mara zote ni cha kweli lakini ipo namna nzuri ya kushughulikia mvutano
kama huo na kusaidia kupata taarifa za kina zaidi zitakazofikia muafaka.
Aidha kwa upande wake Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez ambaye alikuwa mgeni rasmi wa maadhimisho hayo alisema
Tanzania inaongoza Afrika kwa kushindwa kuweka utaratibu mzuri wa
udhibiti mawasiliano.
Alisema
vyombo vya habari ni muhimu katika taifa na hasa kuelekea Uchaguzi Mkuu
wa Taifa unaotarajia kufanyika Oktoba, alisema vyombo vya habari
vinaweza kubomoa au kujenga taifa lolote. "...Waandishi ni watu muhimu
katika kudumisha demokrasia nchini hivyo kuna kila sababu ya kuendelea
kujifunza zaidi.
Maadhimisho
ya uhuru wa vyombo vya habari duniani kitaifa yamefanyika mkoani
Morogoro na kuhudhuriwa na wanahabari mbalimbali, wakongwe, wadau anuai
wa vyombo vya habari huku yakiwa na kauli mbiu ya Usalama wa Vyombo vya
Habari katika Dijitali: Uhandishi Mzuri unaozingatia, Usawa wa Kijinsia
na faragha.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika
la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
akizungumza katika maadhimisho ya Uhuru wa habari duniani yaliyofanyika
mkoani Morogoro. Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani.. Meza kuu katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani.
No comments:
Post a Comment