HALI ILIVYOKUWA TETE LEO KITUO CHA MABASI YAENDAYO MIKOANI-UBUNGO.
Na Bakari Issa,wa Globu ya Jamii-Dar es Salaam.
Mgomo
wa Madereva uliodumu kwa takriban siku moja na ushee, hatimaye umepata
muafaka baada ya Mkuu wa Mkoa wa Kinondoni,Paul Makonda kuusuluhisha kwa
kusaini makubaliano na Uongozi wa Chama cha Madereva.
Makubaliano hayo yaliitaka Serikali kuboresha Mikataba kwa Madereva,malipo kwa madereva hao,pamoja na tatizo la ukaguzi wa magari ili kuondoa usumbufu kwa madereva hao,na kuiomba Serikali kufanya ukaguzi huo kwa siku moja tu.

Akizungumza
na Madereva hao,Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Paul Makonda amewataka
Madereva hao kuachana na mgomo huo na kuwaahidi Madereva hao kuyafanyia
kazi madai yao katika muda ambao wamekubaliana usiozidi saa 4 asubuhi
kesho.
Aidha,Makonda amesema katika madai hayo imeundwa Tume ambayo itashughulikia madai hayo pamoja na kuwahakikishia Madereva hao kuwepo na mwakilishi katika Tume hiyo iliyoundwa,ambayo itajadili masuala ya Mkataba,malipo,matibabu pamoja na suala la kusoma kwa Madereva hao.

Pia,Makonda
amelitaka Jeshi la Polisi kupitia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni
kuwaachia Madereva ambao tayari walikua wamekamatwa kutokana na
kuonekana kufanya fujo katika mgomo huo katika Soko la Urafiki jijini
Dar es Salaam. Kwa Upande wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Madereva,Rashidi
Salehe amemuomba Mkuu wa Wilaya kutatua madai ya Madereva hao ili
kuondoa mgomo ambao unakwamisha usafirishaji wa abiria.
Baadhi
ya Madereva na Makondakta wa Mabasi wanaondelea na Mgomo, wakiwa
wamekaa juu ya Kontena zilizopo kwenye Kituo kikuu cha Mabasi, Ubungo
jijini Dar es salaam kusubiria mustakabali wao, huku ulinzi Mkali wa
Jeshi la Polisi ukiwa umetawala eneo hilo.
Ghafla
likazuka tukio la kurushwa mawe kutoka kwa watu wasiojulikana waliokuwa
nje ya Stendi hiyo na kupeleke watu wote waliokuwa kwenye eneo hilo
kukusanyika sehemu moja ili kujinusuru.
Hali ilikuwa tete pale mawe yalipokuwa yakirushwa, na kupelekea baadhi
ya viongozi pamoja na wanahabari waliokuwepo kwenye eneo hilo
kukusanyika sehemu moja. hivyo polisi walilazimika kutumia mbinu zao na
kufanikiwa kulituliza tukio hilo.
Baadhi
ya Madereva na Makondakta wa Mabasi wanaondelea na Mgomo, wakiwa
wamekaa juu ya Kontena zilizopo kwenye Kituo kikuu cha Mabasi, Ubungo
jijini Dar es salaam kusubiria mustakabali wao, huku ulinzi Mkali wa
Jeshi la Polisi ukiwa umetawala eneo hilo.
Ghafla
likazuka tukio la kurushwa mawe kutoka kwa watu wasiojulikana waliokuwa
nje ya Stendi hiyo na kupelekea watu wote waliokuwa kwenye eneo hilo
kukusanyika sehemu moja ili kujinusuru.
Hali
ilikuwa tete pale mawe yalipokuwa yakirushwa, na kupelekea baadhi ya
viongozi pamoja na wanahabari waliokuwepo kwenye eneo hilo kukusanyika
sehemu moja. hivyo polisi walilazimika kutumia mbinu zao na kufanikiwa
kulituliza tukio hilo.
Baadhi ya wanahabari wakinawa maji kufuaria moshi wa Mabomu ya Machoni yaliyokuwa yakipigwa Ubungo mchana wa leo.
Ulinzi ulitawala eneo lote la Ubungo leo.
Baadhi
ya Madereva na Makondakwa wao wakimzogoa mmoja wa Viongozi wao
alikubali kuzungumza na Viongozi wa Serikali waliofika eneo hilo.
Muda
mfupi baadae, Aliwasili Mbunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa CHADEMA,
Mh. Freeman Mbowe ambaye alipokelewa kwa shangwe na Madereva hao.
Shangwe zikiendelea.
Mmoja wa viongozi wa Madereva akiwasihi wenzake kutulia ili kuwasikiliza viongozi waliokwenda kuwasiliza.
No comments:
Post a Comment