ZANZIBAR INAHITAJI KUENDELEA KUWA SALAMA NA TULIVU-BALOZI SEIF ALI IDDI
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kati Kati
akishindikizwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Said Mohd Dimwa Kulia
yake mara baada ya kuhudhuria Mkutano wa pamoja kati ya Uongozi wa Kampuni inayohusika na
masuala ya Teknolojia ya Kisasa ya mawasiliano ya Baharini { SRT } na watendaji wa sekta ya Habarini
hapo Zanzibar Ocean View.
Afisa Mkuu wa Mradi wa Teknolojia ya Kisasa ya mawasiliano ya
Baharini wa Kampuni ya { SRT } kutoka
Nchini Uingereza Bwana Simon Tucker
akielezea umuhimu wa kifaa cha mawasiliano kinachotumika katika vyombo vya
usafiri Majini kwenye Mkutano wa pamoja na watendaji wa Sekta ya Baharini hapa
Zanzibar.
Wa Pili
kutoka Kulia waliokaa ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi, Kulia ya Balozi ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Said Mohd Dimwa na
wa kwanza kulia ni Bwana Lazaria Moh’d Said.
Balozi Seif akizungumza na
Wanahabari
mara baada ya kuhudhuria Mkutano wa pamoja kati ya Uongozi wa Kampuni
inayohusika na masuala ya Teknolojia ya Kisasa ya mawasiliano ya
Baharini { SRT } ya Nchini Uingereza na watendaji wa Taasisi
zinazohusika na sekta
hiyo hapo Zanzibar.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Zanzibar ikiwa ni sehemu
ya Dunia hii inahitaji kuendelea kuwa
salama na tulivu kutokana na mazingira yake yaliyozunguukwa na Bahari pembe
zote.
Alisema
mfumo wa kisasa wa mawasiliano unaotumika katika mataifa mbali mbali Duniani
uliolenga zaidi katika maeneo ya bahari
yenye kutoa utajiri mkubwa kwa asilimia 90% ya Uchumi wa Dunia unafaa
kutumika ili kuondoa shaka katika udhibiti wa uvamizi wa vitendo vya kiharamia.
Balozi
Seif
Ali Iddi alisema hayo wakati akizungumza na Wanahabari wa Vyombo mbali
mbali
hapa Nchini mara baada ya kuhudhuria Mkutano wa pamoja kati ya Uongozi
wa
Kampuni inayohusika na masuala ya Teknolojia ya Kisasa ya mawasiliano ya
Baharini { SRT } ya Nchini Uingereza na watendaji wa Taasisi
zinazohusika na sekta
hiyo hapo Zanzibar Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar.
Alisema yapo
matukio kadhaa ya uvamizi wa vyombo vya Baharini yaliyowahi kuibuka na kuripotiwa katika ukanda wa Pembe ya Afrika
ambayo yalikuwa yakitekelezwa na maharamia kutokana na udhaifu wa mawasiliano
uliokuwepo wakati huo.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar aliridhika na kukubaliana na Mfumo wa kisasa waTeknolojia
ya mawasiliano ya Baharini unaotumiwa na
Kampuni ya { SRT } ya Nchini
Uingereza katika Mataifa mbali mbali Duniani ambao umesaidia kupunguza wimbi la
uharamia katika maeneo ya Baharini.
Akiwasilisha
mada ya mfumo wa utendaji kazi wa Kampuni hiyo kwenye Mkutano huo Afisa Mkuu wa Mradi wa Teknolojia
ya Kisasa ya mawasiliano ya Baharini wa
{ SRT } Bwana Simon Tucker alisema kifaa maalum cha Mawasiliano huwekwa kwenye chombo
cha Baharini ambacho husaidia kutoa taarifa za mawasiliano.
Bw. Simon
alisema chombo hicho kidogo kinachoweza kuwekwa kwenye boti au hata meli za
uvuvi na abiria kinauwezo wa kusafirisha mawimbi ya mawasiliano kwa zidi ya
meli 40.
Othman
Khamis Ame
Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
No comments:
Post a Comment