VIJANA WA CCM IRINGA WAMPA NGUVU KATIBU WA MKOA HASSAN MTENGA KUKOMBOA JIMBO, LA IRINGA MJINI.
Mtenga katika kikao na baadhi ya vijana hao |
KIU
ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Manispaa ya Iringa kukomboa jimbo la
Iringa Mjini katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu inazidi
kuongezeka, baada ya umoja wake wa vijana (UVCCM Manispaa ya Iringa)
kuahidi kuongeza nguvu ili kuufanikisha mkakati huo.
CCM
ililipoteza jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 kwa Mchungaji
Msigwa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) anayekaribia
kumaliza muda wake.
Katika
kikao kilichozikutanisha sekretarieti za umoja huo kutoka katika kata
zote 18 za manispaa ya Iringa, Mwenyekiti wa UVCCM wa manispaa hiyo,
Kaunda Mwaipyana alisema; “katika kukisaidia chama kushinda uchaguzi
huo, kauli mbiu yetu ni chama kwanza mtu baadaye.”
“Tutapita
katika matawi na kata zetu zote, tutafanya vikao, mikutano ya hadhara
na kuwakumbusha vijana wajibu wa kukipigania chama chao ili mkakati wa
kulikomboa jimbo ufanikiwe,” alisema.
Katibu
wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga aliwaongezea hamasa vijana hao
kwa kuwapa seti 60 za jezi na mipira watakazozitumia kuwahamasisha
vijana hao kupitia mchezo wa soka.
“CCM
ina vijana wengi sana katika jimbo hili, mnahitaji kukutana na
kujipanga, tumieni mbinu zote za kukutana, iwe vikao, mikutano na hata
michezo na ndio maana nimewapa msaada huu,” alisema.
Aliwataka
vijana wa chama hicho kujitokeza kwenye vikao visivyo rasmi vya maeneo
yao wanayoishi na kuitetea CCM kwasababu majibu ya hoja nyingi za
wapinzani wanayo.
Akiwakabidhi
jezi hizo, Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi wa CCM Mkoa wa Iringa, Ephraim
Mhekwa alisema CCM inayo nafasi ya kulikomboa jimbo hilo kama
itajipanga vizuri.
“Pamoja
na kwamba wapinzani walipata viti 65 katika uchaguzi wa serikali za
mitaa wa mwaka jana, wasisahau kwamba CCM ilipata viti 126; hesabu hiyo
inadhihirisha chama chetu kinaungwa mkono mara mbili yao,” alisema.
Aliwataka
vijana hao kuweka bendera za chama hicho kila panapostahili katika
mitaa yote na akawasihi wasikubali kutumika na kukigawa chama kwa maslai
ya wachache.
Naye
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mahamudu Madenge alisema CCM
itaendelea kuwepo hata kama watu wasiotaka kufuata utaratibu wataondoka.
“Wameondoka
wengi, wengine hii leo ni viongozi wa vyama vikubwa vya siasa. Pamoja
na kuondoka kwao CCM ipo pale pale na inaendelea kupata wanachama,”
alisema
|
No comments:
Post a Comment