WAANDISHI ZANZIBAR WAAMIA KUPAMBANA JUU YA HAKIZA WATU WENYE ULEMAVU WA AKILI
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Waandishi
wa habari nchini wameazimia kuboresha Fani ya Uandishi na Utayarishaji
wa Vipindi Vinavyohusu Watu wenye Ulemavu wa Akili ili kuzidi kutetea
Maslahi na Haki za Watu hao.
Maazimio
hayo wameyatoa katika Semina ya Siku mbili ya kuwajengea Uwezo
waandishi hao iliyoandaliwa na Jumuiya ya Watu wenye Ulemavu wa Akili
Zanzibar (ZAPDD) kwa Msaada wa Mwenvuli wa Asasi za Kiraia.
Wamesema
kuna kila haja ya kuboresha Habari na Vipindi wanavyotoa kutokana na
Jamii ya Watu wenye Ulemavu wa akili kukumbwa na Changamoto nyingi na
hivyo kukoseshwa haki zao za Msingi.
Aidha
wameazimia kuongeza Ushirikiano wa karibu baina yao na Jumuiya ya ZAPDD
ili kuona Jamii hiyo inawezeshwa kama zilivyokuwa jamii nyingine
nchini.
Awali
akitoa mada katika Semina hiyo Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Zanzibar
Tunguu Ally Uki aliwataka Wanahabari hao kuwasaidia Walemavu hao wa
Akili kwa kufichua maovu wanaotendewa ili Jamii ipate uelewa na kulinda
haki zao.
“Ndugu
zangu hawa Walemavu wa Akili Hawapewi haki ya Kutoa Ushahidi
Mahakamani, Hawawezi kupiga kura, Wananyanyaswa na Kubakwa hivyo
jitihada zenu ndio zitakazochangia kupata haki zao” Alisema Uki.
Kwa
Upande wake Mdau wa Jumuiya ya ZAPDD Khalid A. Omar ameziomba Taasisi
za Kiraia na Kijamii kuendelea kuihimiza Serikali kuongeza kasi ya
kuzifanyia mapitia Sheria ambazo zinawakandamiza Watu wenye Ulemavu wa
Akili.
Ameongeza
kuwa ni vyema Taasisi hizo pia zisaidie kuishawishi Serikali kutenga
Bajeti ya Angalau Asilimia 5% ya gharama ya Sekta ya Afya ziende kwa
Watu wenye Ulemavu.
Akifunga
Mafunzo hayo Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya ZAPDD Tamrin Ali Said
amesema wamelazimika kufanya kazi na Wanahabari wakiamini kuwa Mchango
wao ni mkubwa katika kusaidia MApambano dhidi ya haki za Watu wenye
Ulemavu wa Akili.
Tunajua
Umuhimu wenu Waandishi ndio tukawaita hapa ingawa kuna Makundi mengine
kama Viongozi wa Dini na Wasanii ambao nao tutafanya kazi kwa pamoja
katika kusaidia kuwapatia haki zao Watu wenye Ulemavu wa Akili.
“Tunakuombeni
sana Mujitolee katika kuandika na kutayarisha Vipindi vyenu ambavyo kwa
hakika Mungu atakulipeni pale mnapofichua Ukandamizwaji wa haki za Watu
wenye Ulemavu wa Akili” Aliomba Makamu Mwenyekiti.
Jumuiya
ya Watu wenye Ulemavu wa Akili Zanzibar ZAPDD kwa sasa ina wanachama
zaidi ya 2,600 ambapo imejikita zaidi katika kutetea haki na fursa Watu
wenye Ulemavu wa Akili nchini.
No comments:
Post a Comment