SHAMY TOURS YA ZANZIBAR YAPATA LESENI YA UTALII SWEDEN
Meneja
Mwendeshaji wa kampuni ya Shamy Tours and Travel Agent Zanzibar, Bw.
Khamis Mwinjuma Simba akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali zinazofanywa
na kampuni hiyo katika sekta ya utalii Zanzibar na Tanzania kwa ujumla
wakati wa zoezi la kugawa zawadi za vinyago kwa wageni waalikwa zaidi ya
300 waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Mgahawa mkubwa unaotoa huduma za
chakula cha Kitanzania unaomilikiwa na mpishi maarufu duniani
mtanzania, Issa Kasuwi Kapande almaarufu kama ‘Chef Issa’ nchini Sweden
katika mji wa Trollhattan.Unaweza kutembelea tovuti yao kwa anauni hii www.shamytours.co.tz
Na Mwandishi Maalumu,Trollhattan, Sweden
KAMPUNI
ya kupokea wageni ya Zanzibar ya Shamy Tours and Travel Agent
Zanzibar, imefungua ofisi nchini Sweden ambayo itakuwa inashughulikia
masuala ya watalii na wageni mbalimbali wanaotaka kuingia Tanzania na
visiwani Zanzibar.
Meneja
Mwendeshaji wa Kampuni ya Shamy, Khamis Mwinjuma Simba akizungumza
mjini hapa alisema kwamba kampuni yake kupitia Bodi ya Utalii ya Sweden
wamepata kibali na leseni ya kuanzishwa kwa branchi ya kampuni hiyo
yenye makao makuu yake mjini Zanzibar , mtaa wa Malindi.
Kampuni
hiyo ambayo tangu kuanzishwa kwake ina miaka minne sasa ilifanya
uzinduzi wa branchi yake hivi karibuni, kazi iliyofanywa na Balozi wa
Tanzania nchini Sweden Dora Msechu wakati akizindua mgahawa wa
Mtanzania, Issa Kapande wiki iliyopita.
Simba
alisema kwamba tangu kuanzishwa kwake wamepata maendeleo makubwa hasa
katika kukabiliana na changamoto za soko na kwamba kwa kuanzishwa kwa
tawi hilo wanaangalia kufikia nchi 30 za Ulaya zinazotumia viza ya
Ulaya.
Alisema
kuwa na ofisi nchini Sweden kumeamsha mori wa kuongeza mafanikio ya
kampuni ili kusaidia juhudi za Wizara ya Utalii Zanzibar katika
kuhakikisha kwamba sekta ya Utalii inaendesha uchumi wa Zanzibar.
Alisema
wizara kama wizara imefanya juhudi kubwa kuhakikisha utalii unakua na
kuleta mafanikio kwa Zanzibar na hivyo ni wajibu wao kama Shamy Tours
kuhakikisha kwamba wanatoa fursa walizowezeshwa na wizara hiyo kutanua
shughuli zao ili kuihakikishia mapato serikali kwa kuingiza wageni wengi
zaidi.
"Tumepata
faida kubwa kama Shamy Tours kutoka kamisheni ya utalii hasa usajili,
kupewa hati za uendeshaji na vipeperushi na machapisho mbalimbali na
hasa chapisho la Karibu Zanzibar linalohusu Zanzibar," alisema Simba na
kuongeza kuwa kwa kusaidiwa huko wameweza kusonga mbele na katika miaka
minne kwa kushirikiana na Issa Kapande, Mtanzania mbaye amefungua
mgahawa wa Kitanzania nchini Sweden, wameweza kuanzisha branchi nchini
Sweden.
Alisema
pamoja na kuzindua ofisi yao, wameitumia siku ya ufunguzi wa mgahawa wa
Issa Kapande kukutana na wadau mbalimbali wa masuala ya utalii nchini
Sweden na kuwapatia zawadi halisi za Kitanzania kuwapa ushawishi wa kuja
nchini.
Balozi
wa Shamy Tours and Travel Agent nchini Sweden, Bi. Anab akitoa maelezo
ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo wakati wa zoezi la
kukabidhi zawadi kwa wageni waalikwa zilizotolewa na kampuni hiyo kwenye
hafla ya uzinduzi wa mgahawa mkubwa unaotoa huduma za chakula cha
Kitanzania unaomilikiwa na mpishi maarufu duniani mtanzania, Issa Kasuwi
Kapande almaarufu kama ‘Chef Issa’ nchini Sweden.
Baadhi ya zawadi hizo ni vinyago vya kimakonde taswira za Wamasai na vipeperushi mbalimbali. Alisema kuwapo kwa Shammy Tours nchini Sweden kutakuza biashara ya utalii.
Alisema
mipango ya kuanzisha ofisi nchini Sweden ilianza zamani wakati Issa
Kapande akifanya shughuli zake katika Hoteli ya African House miaka sita
iliyopita na kushika kasi katika miaka miwili iliyopita ambapo Issa
Kapande alifika Zanzibar mara mbili kukamilisha ushirikiano uliozaa
ofisi hiyo ya Sweden.
Alisema
pamoja na kujitangaza katika nchi zaidi ya 30 za Ulaya kupitia ofisi
hiyo ya Sweden Shamy Tours inatarajia kushiriki katika maonesho ya
utalii Afrika Kusini yatakayofanyika Mei mwaka huu, Urusi Juni mwaka huu
na London, Uingereza Novemba mwaka huu.
Alisema
ushiriki wao ni sehemu ya kutafuta masoko na kuitangaza Tanzania, nchi
ya visiwa vya Zanzibar, mlima Kilimanjaro na mbuga ya Serengeti.
Unaweza kutembelea tovuti yao kwa anauni hii www.shamytours.co.tz
No comments:
Post a Comment