RAIA WAPYA WA TANZANIA WASHANGILIA KUPEWA VYETI VYA URAIA
Raia
wapya wa Tanzania, wakazi wa Kijiji cha Kapemba, Kata ya Mishamo,
wilayani Mpanda, Shukuru Nzokila (kulia) na Anicet Yohanna wakishangilia
baada ya kupokea vyeti vyao vya uraia wa Tanzania, katika Kijiji cha
Ifumbula wilayani humo. Zaidi ya watu 152,572 katika Makazi ya Mishamo,
Katumba na Ulyankulu waliokuwa wakimbizi wa Burundi wa mwaka 1972
walioomba uraia 2008 na kupewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka
2010, wanastahili kupokea vyeti hivyo kama raia wapya wa Tanzania.
Hata
hivyo, Makazi ya Katumba na Ulyakulu tayari wamekamilisha zoezi la
ugawaji wa vyeti hivyo, na sasa ni zamu ya raia wapya wa Makazi ya
Mishamo kuwawiwa ambapo Serikali ya Tanzania inashirikiana na Shirika la
Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR) katika ugawaji wa vyeti
hiyo.
Baadhi
ya raia wapya wa Tanzania, wakazi wa Kijiji cha Kapemba, Kata ya
Mishamo, wilayani Mpanda, wakionyesha vyeti vyao kwa furaha baada ya
kupokea vyeti hivyo vya uraia, katika Kijiji cha Ifumbula wilayani humo.
Zaidi ya watu 152,572 katika Makazi ya Mishamo, Katumba na Ulyankulu
waliokuwa wakimbizi wa Burundi wa mwaka 1972 walioomba uraia 2008 na
kupewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2010, wanastahili
kupokea vyeti hivyo kama raia wapya wa Tanzania. Hata hivyo, Makazi ya
Katumba na Ulyakulu tayari wamekamilisha zoezi la ugawaji wa vyeti
hivyo, na sasa ni zamu ya raia wapya wa Makazi ya Mishamo kuwawiwa
ambapo Serikali ya Tanzania inashirikiana na Shirika la Kimataifa la
Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR) katika ugawaji wa vyeti hiyo.
Kiongozi
wa Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR)
katika Makazi ya Mishamo, Adolph Bishanga akimkabidhi chandarua na
shuka raia mpya wa Tanzania, ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Kapemba, Kata
ya Mishamo, wilayani Mpanda, Ageva Moses (kulia) baada ya kujifungua
mtoto wa kiume wakati akiwa katika kituo cha kupokelea cheti cha uraia
katika Kijiji cha Ifumbula wilayani humo. Licha ya maafisa wa Serikali
pamoja na UNHCR kutoa maelekezo kuwa wagonjwa na wasiojiweza wote
wakiwemo mama wajawazito kusubiria vyeti hivyo nyumbani watakapopelekewa
lakini baadhi ya raia hao wapya wasiojiweza wanafurahia kuja wenyewe
katika vituo vya kupokelea vyeti. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
2.
Mkuu wa Makazi ya Ulyakulu, Abdulkarim Mnacho (kushoto) akimpongeza
raia mpya wa Tanzania, ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Kapemba, Kata ya
Mishamo, wilayani Mpanda, Ageva Moses baada ya kujifungua mtoto wa kiume
wakati akiwa katika kituo cha kupokelea cheti cha uraia katika Kijiji
cha Ifumbula wilayani humo. Licha ya maafisa wa Serikali pamoja na
Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) kutoa
maelekezo kuwa wagonjwa na wasiojiweza wote wakiwemo mama wajawazito
kusubiria vyeti hivyo nyumbani watakapopelekewa lakini baadhi ya raia
hao wapya wasiojiweza wanafurahia kuja wenyewe katika vituo vya
kupokelea vyeti.
Raia
mpya wa Tanzania, ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Kapemba, Kata ya
Mishamo, wilayani Mpanda, Ageva Moses akiwa na mtoto wake mara baada ya
kujifungua mtoto huyo wa kiume wakati akiwa katika kituo cha kupokelea
cheti cha uraia katika Kijiji cha Ifumbula wilayani humo. Licha ya
maafisa wa Serikali pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia
Wakimbizi (UNHCR) kutoa maelekezo kuwa wagonjwa na wasiojiweza wote
wakiwemo mama wajawazito kusubiria vyeti hivyo nyumbani watakapopelekewa
lakini baadhi ya raia hao wapya wasiojiweza wanafurahia kuja wenyewe
katika vituo vya kupokelea vyeti.
Afisa
Uhakiki, Maharusi Nasibu (kushoto) akichukua alama ya vidole kwa raia
mpya wa Tanzania, Mandaakiza Severin kabla ya kupewa cheti chake cha
uraia katika ugawaji wa vyeti hivyo kwa raia wapya zaidi ya 52,565
katika Makazi ya Mishamo yaliyopo wilayani ya Mpanda Vijijini, Mkoa wa
Katavi. Zaidi ya watu 152,572 katika Makazi ya Mishamo, Katumba na
Ulyankulu waliokuwa wakimbizi wa Burundi wa mwaka 1972 walioomba uraia
2008 na kupewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2010,
wanastahili kupokea vyeti hivyo kama raia wapya wa Tanzania. Hata hivyo,
Makazi ya Katumba na Ulyakulu tayari wamekamilisha zoezi la ugawaji wa
vyeti hivyo, na sasa ni zamu ya raia wapya wa Makazi ya Mishamo kuwawiwa
ambapo Serikali ya Tanzania inashirikiana na Shirika la Kimataifa la
Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR) katika ugawaji wa vyeti hiyo.
No comments:
Post a Comment