MAADHIMISHO SIKU YA MALARIA DUNIANI KITAIFA KUFANYIKA MNAZI ,MMOJA JIJINI DAR ES SALAAM.
Mkuu
wa wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa
Mkoa wa Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani
mwaka 2015 alipokutana na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Maadhimisho ya mwaka huu yanalenga kuwakumbusha na kuwaelimisha wananchi
juu ya athari za Malaria na mbinu za kukabiliana na ugonjwa huo.
Tanzania
itaungana na mataifa mengine kuadhimisha Siku ya Malaria duniani Aprili
25 mwaka huu ili kutathmini mafanikio ya utekelezaji wa mikakati
mbalimbali ya kupambana na ugonjwa huo hapa nchini.
Mkuu
wa wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa
Mkoa wa Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani
mwaka 2015, leo jijini Dar es salaam amesema maadhimisho ya mwaka huu
yanalenga kuwakumbusha na kuwaelimisha wananchi juu ya athari za ugonjwa
wa Malaria na mbinu za kukabiliana na ugonjwa huo.
Amesema
maadhimisho hayo kitaifa yatafanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja
jijini Dar es salaam chini ya kauli mbiu isemayo Wekeza kwa Maisha ya
Baadaye, Tokomeza Malaria huku msisitizo mkubwa ukilenga kuikumbusha na
kuielimisha jamii kuepuka athari na madhara yanayotokana na ugonjwa
huo.
Bw.
Mushi amesema maadhimisho ya mwaka huu yamelenga kuwaelimisha wananchi
juu ya umuhimu wa kutambua dalili za malaria na kuwahi kwenye vituo vya
kutolea huduma pindi wasikiapo dalili za ugonjwa huo ili waweze kupima
afya zao na kupatiwa matibabu.
“Ugonjwa
wa malaria kwa muda mrefu umekuwa na athari kwa nguvu kazi ya taifa na
utekelezaji wa mikakati mbalimbali, hivyo ni wajibu wetu kushirikiana
kuwaelimisha wananchi kuwahi katika vituo vya afya pindi wasikiapo
dalili za malaria” Amesema.
Kwa
upande wake Mkuu wa Kitengo cha Uhamasishaji Mpango wa Udhibiti wa
Maambukizi ya Malaria Dkt. Linda Nakara akizungumza kuhusu maadhimisho
hayo amesema kuwa maadhimisho ya mwaka huu yataambatana na wadau
mbalimbali wa huduma za afya kufanya maonyesho ya huduma wanazotoa kwa
jamii.
Ameongeza
kuwa wadau hao pia wataendesha shughuli za uchunguzi wa vimelea vya
malaria kwa kutumia vipimo vinavyotoa majibu kwa haraka (MRDT) na
matibabu ya ugonjwa wa malaria kwa wale watakaogundulika kuwa na
malaria.
No comments:
Post a Comment