MASHABIKI WA SIMBA UKAWA WAPATA AJAKI,YADAIWA WATU WATANO WAMEPOTEZA MAISHA
kikundi
cha ushangiliaji cha tawi la Simba la Mpira na Maendeleo maarufu kwa
jina la Simba Ukawa wamepata ajali iliyotokea leo mjini Morogoro
wakielekea mjini Shinyanga kuisapoti timu yao inayocheza mechi ya ligi
kuu kesho dhidi ya Kagera Sugar.
Taarifa mpya na za uhakika zinasema watu watano (5) akiwemo kiongozi wa
Simba Ukawa, Mohammed Kingolile ‘Ngumi Jiwe’ wamefariki dunia na watu 15
wapo mahututi.
Ajali hiyo imetokea eneo la Mvomero ikihusisha basi dogo aina ya Toyota
Costa lililopinduka na kuacha njia. Polisi bado hawajatoa tamko rasmi.
Waliotangulia mbele ya haki mpaka sasa ni:
Waluya, Rehema, Ali Kingolile ‘Ngumi Jiwe’ Wabi na dereva wa gari Abdallah Fundi.maandishi picha na Shafih dauda.com



No comments:
Post a Comment