KATIKA KUELEKEA KUPATA TAIFA SALAMA KIMTANDAO
Taarifa “INAYOSOMEKA HAPA”
ilitolea ufafanuzi wa Nchi ya India inavyo pambana ili kuweza kufikia
malengo katika kuboresha usalama mitandao hasa katika wizi unaofanywa
kupitia ATM. Na baada ya kupata kutolea ufafanuzi muswada wa sharia
mtandao, taarifa “INAYOSOMEKA HAPA”
Ilifafanua yamuhimu kuzingatia ili sheria hiyo iweze kupelekea
kufikiwa kwa malengo kusudiwa ya kupata Tanzania salama kimtandao na
kupunguza wimbi la makosa mtandao nchini.
Baada
ya hayo nilipata kuhudhuria mikutano kadhaa katika nchi mbali mbali
ambapo nilifanikiwa situ kuwasilisha mada kwa wataalam wengine wa
maswala ya usalama mitandao bali pia kujifunza mengi kutoka kwao katika
maswala mbali mbali ya msingi ya kufanyiwa kazi ili kuweza kuboresha
usalama mitandao situ katika ngazi ya kitaifa bali na kibara pamoja na
Dunia kwa ujumla.
Makubwa
matatu ambayo nimeona niyazungumzie leo ni pamoja na kuhakiki kuna njia
madhubuti na zenye mpango stahiki za kukuza ulewa kwa watumiaji
mitandao jinsi ya kujilinda na kulinda wengine watumiapo mitandao,
Kuhakikisha Taifa linakua na mikakati endelevu ya kutengeneza na
kuongeza uwezo wataalam wa maswala ya usalama mitandao pamoja na
kupatikana na ufumbuzi wa kudumu wa kukabiliana na wimbi la wizi wa
fedha kupitia mashine za ATM.
No comments:
Post a Comment