Habari
zilizotufikia punde zinaeleza kuwa watu kadhaa ambao idadi yao bado
haijafahamika, wanasemekana wamepoteza maisha baada ya basi la abiria
liitwalo Nganga linalofanya safari zake kati ya Iringa na Kilombero
kugongana uso kwa uso na lori aina ya Fuso na kisha magari hayo
kuteketea kwa moto maeneo ya milimani kilomita kadhaa kutoka Ruaha
Mbuyuni kuelekea Morogoro, majira ya saa mbili asubuhi leo. Pichani ni
basi hilo la Nganga wakati na bada ya kuteketea kwa moto. Tunaendelea
kufuatilia taarifa hizi na tutazileta mara zitapopatikana.
|
No comments:
Post a Comment