Header Ads

WADAU WA MWANAHARAKATI MZALENDO MEDIA WAJITOA KUWAFARIJI WAZEE WASIOJIWEZA



Mkurungezi mtendaji wa Mwanaharakati Mzalendo Media  Krantz Mwantepele akisaini kitabu cha wageni  mara baada ya kufika katika kituo cha wazee wasiojiweza Msimbazi  kinachosimamiwa na jimbo kuu hapa dar es salaam kanisa la katoliki na kuhudumia wazee
wapatao kumi na moja waliokuwa wanaishi katika mazingira magumu.Timu nzima ya Mwanaharakati Mzalendo Media ilikuja hapa kuwaona wazee hawa na kupata nafasi ya kuwafariji na kutoa baadhi ya misaada ya chakula na nguo za kuwasitiri leo siku ya jumamosi tarehe 7/3/2015.

Mdau Marko Mlonganile akipata nafasi ya kumsalimia mmoja ya wazee wanaopatikana katika kituo hiki na kupata nafasi ya kujua baadhi ya changamoto zinazopatikana katika kituo hiki siku ya jumamosi tarehe 7/3/2015.
Mdau subilaga james akiwa  katika taswira na mmoja bibi wanaopatikana katika kituo hiki cha wazee wasiojiweza kinachosimamiwa na jimbo kuu Dar es salaam la kanisa katoliki na kuweza kuhudumia wazee wapatao  kumi na moja   siku ya jumamosi tarehe 7/3/2015.

No comments:

Powered by Blogger.