Viongozi wa Dini waaswa kuhubiri amani na utulivu kuelekea mchakato wa Katiba Mpya
Mkuu
wa Wilaya ya Mjini Magharibi Bw.Ayoub Mohamed Mahmoud akiongea na
Viongozi mbalimbali wa Dini na kuwataka kuhubiri amani na utulivu hasa
katika kipindi hiki cha kuelekea upigaji kura ya maonikwa Katiba
Inayopendekezwa pamoja uchaguzi Mkuu
Mbunge
wa WAWI kupitia chama cha wananchi CUF Mh. Hamad Rashid Mohamed
akiongea na viongozi wa Dini mbalimbali na kuwaasa kuisoma, kuielewa
Katiba Inayopendekezwa na kuacha kupotoshwa kwa kusomewa vipengele vya
Katiba hiyo bila kupewa ufafanuzi, wakati wa mkutano ulioratibiwa na
Kamati ya Amani na Utulivu Tanzania kushirikisha viongozi wa Dini leo
Zanzibar.
Katibu
wa Kamati ya Amani na utulivu Tanzania Padri. Damas Mfoi akiongea
katika mkutano wa Kamati ya Amani na Viongozi wa Dini mbalimbali
Zanzibar na kuwaasa kusambaza ujumbe wa Amani na kuepuka mambo yoyote
yatakayoashiria uvunjifu wa amani hasa katika kipindi hiki Taifa
likielekea katika Mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya na Uchaguzi
Mkuu.
Baadhi ya Viongozi mbalimbali wa Dini Zanzibar wakifuatilia Mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika Mkutano huo
Mmoja ya Mjumbe wa Mkutano akifanya rejea katika Katiba Inayopendekezwa wakati wa uwasilishwaji wa Mada katika Mkutano huo.
(PICHA NA HASSAN SILAYO)
No comments:
Post a Comment