UKEKETAJI BADO NI TATIZO SUGU TANZANIA,LHRC NA MASHIRIKA MENGINE WATOA NENO NZITO,SOMA HAPA
Mwanasheria
kutoka kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC ndugu HAROLD SUNGUSIA
akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam juu ya siku ya
kupinga ukeketaji duniani
|
NA EXAUD MTEI
Ikiwa
leo ni siku ya kupinga vitendo vya ukeketaji duniani imeelezwa kuwa
bado mapambano dhidi ya ukatili huo hapa nchini kwetu Tanzania
yanahitaji nguvu ya ziada kwani bado baadhi ya mikoa imekuwa sugu katika
vitendo hivyo ambapo serikali imetakiwa kuchakua hatua mara moja juu ya
watu ambao wanahusika katika vitendo hivyo.
Akizungumza
na wanahabari leo mwanasheria kutoka kituo cha sheria na haki za
binadamu LHRC akiwakilisha mashirika zaidi ya 15 yanayohusika na
ukeketaji nchini Tanzania wakili HAROLD SUNGUSIA amesema kuwa mwaka 2014
umeshughudia watoto wengi wakikeketa, pamoja na jitihada za kutokomeza
vitendo hivyo ambapo ametolea mfano wilaya ya tarime pekee takribani
watoto 1400 walikeketwa na watoto hao ni kutoka katika koo za bukira
watoto 212,bukenye watoto 230,iregi watoto 800,pamoja na nyabasi watoto
160,ambapo ni idadi kubwa sana na ikizingatiwa kuwa ni wilaya moja tu.
IMELDA
URIO ambaye ni mkurugenzi wa uwajibikaji na uwezeshaji kutoka kituo cha
sheria na haki za binadamu LHRC akizungumza na wnahabari
|
Amesema
kuwa pamoja na kuwepo kwa sheria zinazolikemea tatizo hilo bado cha
kusikitisha ni kuwa mila hii imekuwa ikitekelezwa kwa kasi sana katika
maeneo mbalimbali nchini Tanzania katika baadhi ya jamii zetu.
“tunaitaka
serikali kwa kupitia jeshi la polisi kusimamia sheria na kuwachuklia
hatua za kisheria watu wote watakaobainika kufanya vitendo hivi”amesema
SUNGUSIA
Ameongea
kuwa ukeketaji ni kosa la jinai, na kosa la jinai huwa haliishii yani
halina ukomo wa muda hivyo wanatarajia kuwa kama serikali inamaanisha
kweli kupinga ukeketaji huo basi iweze kufwatilia huko vijijini na
kuwabaini wale wote wanaoshiriki kukeketa watoto na kuwachukulia hatua
stahiki
Mwakilishi
kutoka chama cha wanahabari wnawake tanania TAMWA bi GOGFUDA JOLA
akizngumzia kuhusu shirika lao linavyoshgulikia tatizo la ukeketaji
katika maeneo mbalimbali nchini.
|
Wasaka habari wakiwa wanasikiliza kwa makini
|
Aidha
mashirika hayo yanayotetea na kupinga vitendo vya ukeketaji wamewaomba
wadau wengine na watanzania kwa ujumla kujiuga kwa pamoja kupinga
vitendo hivyo kwani ni vitendo vya kikatiki kwa mtoto wa kike na ni
kumnyima haki zake za msingi kama mwanadamu,ikiwa ni pamoja na kutoa
elimu zaidi juu ya madhara ya ukatili huo.
Baadhi
ya mashirika ambayo leo wameungana kwa pamoja kupinga vitendo hivyo ni
TAWLA,TAMWA,DIAC,CCT,WORD VISSION,NAFGEM,AFNET,WOWAP, CDF,WLAC,TGNP MTANDAO,WILDAF,BAKWATA,TGNP pamoja na HOUSE OF PEACE.
TAMKO NZIMA LIKO CHINI
No comments:
Post a Comment