Benki ya Exim yaadhimisha Siku ya Saratani Duniani na Watoto wenye Saratani Hospitali ya Taifa Muhimbili
Meneja
masoko msaidizi wa Benki ya Exim, Bi. Anita Goshashy akishikana mikono
na Dr. Livin Mumbari Daktari wa watoto katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili, muda mfupi baada ya benki hiyo kukabidhi vifaa mbalimbali kwa
watoto waliolazwa hospitalini hapo kwenye wodi maalum ya watoto
wanaougua ugonjwa wa saratani katika kuadhimisha siku ya saratani
duniani.
Wanaoshudia ni baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Exim na wazazi
wa watoto hao. Benki hiyo ilikabidhi vifaa mbalimbali vikiwemo vyakula,
vifaa vya kuchezea, sabuni, vifaa vya shule nk, lengo likiwa ni kujenga
uelewa kuhusiana na ugonjwa wa saratani mpango unaoendana na kauli mbiu
ya mwaka huu ya Siku ya Saratani Duniani inayosema kuwa tatizo la
saratani “lipo ndani ya uwezo wetu”.
No comments:
Post a Comment