Header Ads

WATU 36 WAMEFARIKI NA WENGINE 46 KUJERUHIWA HUKO SHANGHAI CHINA WAKATI WAKIUSUBIRIA MWAKA MPYA




Shanghai China1
Umati wa watu jijini Shanghai ukiwa eneo la tukio wakati wakisubiria mwaka mpya
Sherehe za kuukaribisha mwaka mpya zimeingia dosari huko China katika mji wa Shanghai ambapo mamia kwa maelfu ya washerekeaje waliojawa furaha na shauku walikuwa wamekusanyika katika uwanja maarufu unaotazamana na bahari ambapo ghafla sherehe tarajiwa ikaleta majanga.
Watu katika umati huo walianza kukanyagana, tukio ambalo lilisababisha vifo vya watu 36 na wengine 46 kujeruhiwa vibaya.
Habari zimeeleza kuwa chanzo cha mkanyagano huo unadhaniwa kuwa ni tamaa ya kugombania kujipatia fedha ambazo watu walihisi kuwa zimedondoshwa katika dirisha la ghorofa moja lililokuwepo katika uwanja huo.
Fedha hizo zilikuwa ni noti bandia zenye umbile na mfano wa dola . 
Miongoni mwa waliouwawa pia wamo watoto na wale waliojeruhiwa waliwahishwa katika hospitali za karibu na jiji la Shanghai na waliohojiwa walieleza tafrani mbaya ya mkanyagano iliyojitokeza na kufadhaisha umati.

2459C0E700000578-2892994-image-a-50_1420062028410
Palikuwa hapatoshi
2459C12900000578-2892994-image-a-51_1420062037704
Wakazi wa China wakiwa wamekusanyika jijini Shanghai sehemu palipotokea vifo vya watu 36 kwa kukanyagana
2459C20500000578-2892994-image-a-49_1420061775678
Gari la wagonjwa likijaribu kupenya kwenye msururu wa watu kwa ajili ya kwenda kuwabeba majeruhi na wahanga wa tukio hilo
2459D16500000578-2892994-image-a-56_1420063119626
Ndugu waliopoteza wapendwa wao wakifarijiana
eneo la tukio
Wakazi wa Shanghai wakiweka mashada ya maua eneo palipotokea vifo
Majeruhi wa shanghai
Muhanga akiwa kwenye baiskeli maalum baada ya kunusurika
mashada ya maua Shanghai Mwanama akilia Shanghai  Shanghai1

No comments:

Powered by Blogger.