Header Ads

Soma Salaam Za Salamu za Mbunge wa Nzega -CCM Dr. Hamisi Kigwangalla kwa Watanzania , Mwaka Mpya 2015




 Mbunge wa Nzega -CCM Dr Hamisi Kigwangalla
---
Ni Mwaka Mpya Tena! Dr. Hamisi Kigwangalla, MB.
Ndugu Watanzania wenzangu,
Kwa heshima na taadhima na kwa moyo wa kiutumishi, najisikia furaha kuwatumia salamu za Mwaka mpya 2015. Kwa hakika Mungu amekuwa mwema sana kwangu na kwako mwaka 2014 kwa namna nyingi mbalimbali, ila kwa kiasi kikubwa kwa kutujalia zawadi ya uhai, mafanikio kwenye kazi zetu, uvumilivu tulipoanguka, nguvu tulipokutana na changamoto mbalimbali, na uwezo wa kupambana nazo tulipolazimika kufanya hivyo, na zaidi kwa kutusimamisha pamoja kwenye kamba ya mshkamano wa kitaifa kwa sisi sote kama watanzania.

Kwa niaba ya wanaNzega, familia yangu, marafiki na ndugu zangu wa‪#‎TeamBelieve‬, naomba nitumie fursa hii kuelezea hisia na fikra zangu za Tanzania tunayoitaka kwa Taifa letu zuri, ambalo mimi na wewe tunaita nyumbani kwetu.

No comments:

Powered by Blogger.