STARTIMES YAZINDUZI KIFURUSHI KIPYA CHA NYOTA

Meneja Mauzo wa StarTimes Tanzania,
David Kisaka (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani), Dar es Salaam leo asubuhi wakati wa uzinduzi wa bei mpya ya
king’amuzi kitakakochouzwa kwa sh. 4000 sambamba na kifurushi kipya cha
Nyota cha malipo ya sh. 4000 kwa mwezi, Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na
Mauzo wa StarTimes Tanzania, Jacky Yu. Bei hiyo mpya ya king’amuzi na
kifurushi itamfanya mteja afurahie chaneli zisizopungua 16 ikiwa 9 ni za
kimataifa na 7 za nyumbani kwa muda wa miezi saba na nusu.

Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa StarTimes Tanzania, Jacky Yu (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.

Baadhi ya wateja wakiangalia chaneli mbalimbali zinazorushwa na StarTimes kupitia vifurushi vyao mbalimbali.
…………………………………………………………………………………
KAMPUNI ya StarTimes Tanzania ambayo
inatoa huduma bora na nafuu za matangazo ya digitali imezidi kupanua
huduma zake baada ya kuja na kifurushi kipya na bei mpya ya king’amuzi kwa sh. 4000/- tu gharama ambayo ni ya chini kabisa kutowahi kutokea nchini.
Akizungumza katika mkutano na waandishi
wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu huduma hiyo mpya Mkurugenzi wa
Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Star Media Tanzania ambao ni wauzaji wa
ving’amuzi vya StarTimes nchini, Jacky Yu amebainisha kuwa uzinduzi huo
ni sehemu ya kutimiza ahadi kwa watanzania kwamba watakuwa wakitoa
huduma bora na kwa bei nafuu ambayo kila mtu ataweza kuimudu.
“Leo tunayo furaha kubwa kabisa
kuwatangazia umma wa watanzania kwamba StarTimes imeshusha bei ya
king’amuzi chake mpaka kufikia sh. 4000 na kuzindua kifurushi kipya na
cha bei ya chini kinachokwenda kwa jina la NYOTA ambacho kitapatikana
kwa malipo ya sh. 4000 kila mwezi.”
“Kifurushi hiki kipya cha NYOTA kina
jumla ya chaneli zisizopungua 16, saba ni za nyumbani na 9 ni za
kimataifa ambazo ni Star Swahili, Bollywood Swahili, E-Star, Star Music,
Kungfu 1, Child Smile, TBN, TV Imani na CCTV News. Ili mteja aweze
kuunganishwa na kifurushi hiki itabidi aambatanishe na malipo ya awali
ya shilingi 30,000 na kuweza kufaidi kwa muda wa miezi saba na nusu.”
Alifafanua zaidi, Yu
Yu alisema kuwa, baada ya muda wa ofa
iliyotolewa kwa wateja wa kifurushi kipya cha NYOTA kuisha, mteja
ataamua kama anaendelea na kifurushi hiki cha kulipia sh. 4000 kila
mwezi au kutazama vingine vya kawaida. Ili mteja kurudishwa katika
vifurushi vya kawaida ambavyo vitamruhusu kutazama chaneli za bure za
nyumbani na kulipia vifurushi vilivyopo basi itambidi afuate njia ya
kawaida ya kujiunga ambayo ni rahisi kwa kupiga *150*63# na kufuata
maelekezo au atembelee ofisi zetu na za mawakala.
“Madhumuni makubwa ya bei hii mpya ya
king’amuzi na kifurushi cha NYOTA ni kumtaka kila mtanzania hata Yule wa
kipato cha chini aweze kupata matangazo ya dijitali. Tuna imani kubwa
kwamba kifurushi hiki kipya kitakidhi mahitaji ya wateja wetu wote ambao
wanapenda huduma zetu lakini hushindwa kulipia gharama za vifurushi
vilivyopo.” Alisema Bw. Yu na kumalizia, “Siku zote StarTimes
tutaendelea na dhamira yetu ya kutoa huduma za uhakika na kwa bei nafuu
ili kumfikia kila mteja. Tunaimani matangazo ya dijitali ni fursa ambayo
kila mtanzania lazima anufaike nayo.”
Kwa upande wake Meneja Masoko wa
kampuni hiyo, David Kisaka aliongezea kwa kusema, “kifurushi hiki kipya
kimeongezewa katika vifurushi vyetu vilivyopo, hivyo basi kuanzia leo
hii tutakuwa na jumla ya vifurushi vinne ambavyo ni NYOTA, Mambo, Uhuru
na Kili. Tulichoongezea ni unafuu na kuwajali wateja wetu kwani
tunatofautiana kwa hali za kiuchumi na tunafahamu kwamba watanzania
wengi ambao ni wateja wanavipato vya kawaida. Tunaamini kwa kifurushi
hiki kipya cha NYOTA sasa tutawafikia watanzania wote na kuwawezesha
kufurahia matangazo ya dijitali.”
“Ningependa kutoa wito kwa wateja wetu
kutembelea maduka yetu na ya mawakala wetu popote yalipo ili kuweza
kuhudumiwa au kupiga namba ya huduma ya wateja ambayo ni 0764 700 800
ili kupata maelezo na ufafanuzi zaidi. Na pia ningependa kuwatoa hofu
huduma hii ni endelevu kwani ni mwanzo tu wa maboresho ya huduma zetu
kwani kuna mabo mazuri lukuki yapo njiani yanakuja. Na kwa wale wasio
wateja wetu basi huu ndio muda muafaka kwa wao kuunganishwa na huduma
zetu, wameshapitwa na mengi lakini hili si la kuliacha lipite hivi
hivi.” Alihitimisha Kisaka.
No comments:
Post a Comment