RAIS MUGABE AMTIMUA KAZI MAKAMU WAKE
Rais
wa Zimbambwe Robert Mugabe amewafukuza kazi mawaziri wake wawili na
manaibu waziri wapatao watato, hatua ambayo imemkumba aliyekuwa makamo
wake Joyce Mujuru.
Hatua hii ya kuwafuta kazi mawaziri wake inafuatia hali tete
ya kisiasa nchini humo na kujiandaa na lolote litakalotokea lakini pia
ni kutokana na mafanikio hafiifi ya kiongozi uyo mwenye umri wa miaka 90
endapo atajiuzulu ama kufa.
Mugabe ambaye siku za hivi karibuni ameamua kupumzika katika
msimu huu wa sikukuu na kuchagua kwenda katika bara la Asia kupumzika
yeye na familia yake.
Wadadisi wa mambo nchini zimbabwe wanasema mafaniko ya Rais
uyo hayakutarajiwa na walio wengi, pia anasema hofu ya kupokwa madaraka
aliyonayo Rais Mugabe ilimsukuma kumtimua kazi makamu wa Rais wake bi.Joyce Mujuru aliyekuwa akipata umaarufu mkubwa kisiasa nchini mwake.
Mujuru aliingia katika kashfa ya kutaka kumuua Rais lakini
pia anashtumiwa kwa kukigawa chama cha ZANUPF na lingine ni kushindwa
kwake kufunga mikataba ya kibiashara.
Kufuatia tuhuma hizo nafasi ya Bi.Mujuru ilichukuliwa na
waziri Emmerson Mnangagwa ambaye ni mshirika wa miaka mingi wa Rais
Mugabe na mmoja kati ya viongozi maarufu sana nchini Zimbabwe.

No comments:
Post a Comment