MAUAJI TENA!!! KIJANA MWINGINE MWEUSI AUWAWA KWA KUPIGWA RISASI NA AFISA POLISI MJINI MISSOURI
Uhasama baina ya mapolisi na watu weusi umeonekana kuendelea
kushika kasi baada ya kijana mwingine mweusi kuripotiwa kuuwawa kwa
kupigwa risasi na afisa polisi usiku wa Jumanne(Dec.23) kwenye kituo kimoja cha gesi kilichopo eneo la Berkeley, Missouri nchini Marekani.
Vyombo vya habari vimemnukuu msemaji wa Idara ya polisi wa St.Louis,
Sajenti Brian Schellman katika taarifa yake akisema afisa huyo wa
polisi alikuwa katika kituo cha gesi kilichopo katika kitongoji cha St.Lous
na alipogundua akifuatwa na watu wawili, mmoja wao akidaiwa kuwa na
silaha mkononi , afisa aliwafyatulia risasi na kumuua kijana uyo hali
iliyopelekea mwenzake kutimua mbio.
Wakati polisi wakikataa kutaja jina la muhanga wa tukio hilo,
mwanamke ambaye alitambuliwa na vyombo vya habari kwa jina la Toni
Martin alikiambia kituo cha NBC kuwa marehemu ni mtoto wake wa kiume
anayeitwa Antonio Martin mwenye umri wa miaka 18 na kudai mwanae
alitoka kwenda kumtembelea mpenzi wake.
”Aliondoka nyumbani kwenda kumuona mpenzi wake. Labda alianza kukimbia na wao wakampiga risasi”, alisema Toni huku akitokwa na machozi na kuongeza kwamba hafikirii kama mtoto wake alibeba silaha.
Toni martin aliongezea kwa kusema mpenzi wa mtoto wake ndiye
aliyemjulisha kuhusu shambulio la risasi na kumpeleka hadi eneo la tukio
na kukuta maandamano makubwa ya Raia wakipinga vikali mauaji hayo.
Hivi karibuni kumekuwepo na mfululizo wa matukio ya vifo vya
watu weusi kuuwawa kwa kupigwa risasi na maafisa polisi wazungu nchini
marekani hali inayopelekea kuchochea vitendo vya kibaguzi na uadui
mkubwa baina ya matabaka hayo mawili.
Miongoni mwa vifo vya watu weusi vilivyowahi kuvuta hisia za
watu wengi nchini humo ni pamoja na kifo cha Trayvon Martin, Eric
Garner, Mike Brown na kijana Ismaaiyl Brinsley aliyejitoa muhanga kwa
kuwauwa kwa risasi maafisa wawili wa polisi na kisha mwenyewe kujimaliza
mjini Brooklyn.






No comments:
Post a Comment