PICHA NA HABARI KUTOKA OFISI YA RAIS,TUME YA MIPANGO:KIWANDA CHA SUKARI KAGERA CHAZALISHA ZAIDI
Timu
ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
wakioneshwa kwa vitendo matrekta yanayotumia setalaiti kusawazisha shamba kwa ajili ya uzalishaji
miwa.
Timu ya
Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
wakioneshwa mashine ya kumwagilia maji miwa ijulikanayo kwa kitaalamu kama Centre Pivot System.
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya
Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikikagua mitambo ya kuzalishia
sukari katika Kiwanda cha Sukari cha Kagera.
Kiongozi wa
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango,
Bibi Florence Mwanri (Mwenye kofia ya bluu) akionja sukari inayozalishwa na Kiwanda cha Sukari cha Kagera. Kushoto ni Mratibu wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi
ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Senya Tuni.
Meneja wa Kiwanda cha Sukari cha
Kagera, Bw. Ashwin Rana (Kulia) akiwaonesha Wakaguzi wa Miradi
ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango mashine mpya
zinazotumika kuvutia maji kwa ajili ya kumwagilia miwa.
Msimamizi Mkuu wa Mtambo wa maji wa
Kiwanda cha Sukari cha Kagera, Mhandisi Abdul Adinani (Kulia) akitoa maelekezo
ya namna ya maji yanavyochujwa kabla ya kutumika kwa ajili ya umwagiliaji wa
miwa. Wanaomsikiliza ni Wakaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Mtaalamu
wa uchongaji na usawazishaji
wa ardhi kwa ajili ya mashamba ya miwa, Mhandisi Ali Khamis (Kulia)
akitoa
maelezo ya namna matrekta yanayotumia setalaiti (hayapo pichani)
yanavyofanya
kazi. Wanaomskiliza ni Prof. Longinus Rutasitara (Kushoto) ambaye ni
Naibu Katibu
Mtendaji anayeshughilikia masuala ya Uchumi Jumla na Katikati ni
Kiongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais,
Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri.
No comments:
Post a Comment