Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais,Mh.Ummy Mwalimu afanya ziara ya ukaguzi wa mazingira kiwanda cha Ok Plastic jijini Dar
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu
amefanya ziara ya ukaguzi wa mazingira katika kiwanda cha OK Plastic
kilichopo jijini Dar Es Salaam. Ziara hiyo ni muendelezo wa ziara za
kuangalia hali ya mazingira kwenye viwanda mbalimbali hapa Nchini.
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu akipata maelezo
ya uendeshaji wa kiwanda cha OK Plastic kutoka kwa Menejimenti ya
kiwanda hiko.Wengine wanaofuatia ni Mkurugenzi Msaidizi-Mazingira Ofisi
ya Makamu wa Rais bi Magdalena Mtenga, Bwana Anacleto Pereira Mkuu wa
Idara ya sheria wa OK plastic, Fadl Ghaddar Mkurugenzi Mtendaji wa OK
plastic na Martin Msamba Meneja wa kiwanda.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu
akimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bi
Magdalena Mtenga wakati wa ziara hiyo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalimu akiangalia jinsi betri chakavu zinavyohifadhiwa kiwandani hapo.
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Ummy Mwalim akielekeza jambo
wakati wa ziara ya kutembelea kiwanda cha OK Plastic kilichopo jijini
Dar Es Salaam
No comments:
Post a Comment