Bodi ya Filamu Tanzania yaifagilia tamthilia ya Siri ya Mtungi

Bodi ya Filamu Tanzania imewataka
waandaaji wengine wa fani hiyo kuiga mfano wa waandaaji wa tamthilia ya Siri ya
Mtungi, Shirika Lisilo la Kiserikali (NGO ya Media for Development
International Tanzania (MFDI-TZ) kwa kutoa filamu yenye mafundisho mbali ya
kuburudisha.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji
wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fissoo kupitia kwa mwakilishi wake, Beatrice
Sumari kwenye ukumbi wa Cinemax Century wakati wa uzinduzi rasmi uliowashirikisha
wadau wa fani hiyo, wadhamini na waandaaji.
Sumari alisema kuwa Tamthilia ya Siri ya
Mtungi Msimu wa Pili mbali ya kuburudisha, pia imetoa ajira kwa Watanzania
wengi, pia imeleta changamoto kuhusiana na mabadiliko ya tabia kwa jamii.“Filamu imetengenezwa kwa ubora wa hali
ya juu, hii ni fursa kwa wadau wa fani hiyo kuiga MFDI-Tanzania kwa kuleta
katika jamii filamu yenye ubora huu, naomba wengine wafuate nyayo zao,” alisema
Sumari.
“Filamu hiyo ina ubora wa picha, sauti, maudhui na mfuatano wa
matukio wa kipekee na kuleta burudani ya aina yake.. ni tamthilia ambayo
ukianza kuangalia, hauta kinai na kuwa na hamu ya kufuatilia kile kinachofuata,”
alisema.Afisa kutoka Taasisi ya Misaada ya
Wamarekani kupitia (Usaid), Ana Bodipo alisema kuwa wanajisikia furaha
kudhamini tamthilia hiyo ambayo imezungumzia maisha halisi ya Mtanzania.
Bodipo alisema kuwa alisema kuwa
tamthilia hiyo inaelekeza jamii kuhusiana na ugonjwa hatari wa Ukimwi na kwa
wao ni moja ya nyenzo ya kushiriki katika masuala ya afya katika maeneo
mbalimbali nchini.
“Matukio mengi katika tamthilia hii yana
akisi taswira ya kweli katika jamii na na kuwafanya wafuatiliaji kupata somo
halisi kutokana na changamoto mbalimbali,” alisema Bodipo.Mtayarishaji wa tamthilia hiyo, Louise Kamin
kutoka taasisi ya Media for Development International Tanzania (MFDI-TZ) alisema
kuwa wamefuraishwa na mapokeo ya tamthilia hiyo pamoja na kuhitimisha na
kufichua kilichopo katika mtungini.
alisema kuwa sehemu ya pili ya tamthilia
hii inakamilisha Siri ya Mtungi kufuatia msisimko mkubwa wa msimu wa kwanza.Kamin alisema kuwa kukamilika kwa hatua
ya pili kunatokana na udhamini mnono wa the John Hopkins University Centre for
Communication Programs (JHU CCP) ambao walitoa uongozi wa elimu na mkakati
katika tamthilia, taasisi ya Misaada ya Wamarekani kupitia (Usaid), Wizara ya
Afya Ustawi wa Jamii na MFDI.
No comments:
Post a Comment