WAHISANI WA MAENDELEO KUTOKA MAREKANI WAZINDUA MIONGOZO YA KUPAMBANA NA MAGONJWA YA MAAMBUKIZI ZANZIBAR
Mkurugenzi
wa Mradi wa kudhibiti na kuzuia maambukizi ya magonjwa unaosimamiwa na
Shirika la Afya la Kimataifa la Jhpiego Dkt. Albert Komba (alisimama)
akitoa maelezo katika uzinduzi wa Miongozo ya kitaifa ya kukinga na
kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya magonjwa katika sherehe zilizofanyika
Wizara ya Afya Mjini Zanzibar.
Kaimu Mkurugenzi Wizara ya Afya Dkt. Jamala Adam Taib akizundua vitabu viwili vya miongozo ya Kitaifa ya kukinga na kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya magonjwa katika Hospitali na sehemu za kutolea huduma za Afya katika sherehe zilizofanyika Wizara ya Afya Mjini Zanzibar.
Dkt. Jamala Adam Taib akionyesha vitabu vya
miongozo ya Kitaifa ya kukinga na kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya
magonjwa katika Hospitali na sehemu za kutolea huduma za Afya.
Meneja
Mradi wa kudhibiti na kuzuia maambukizi ya magonjwa Zanzibar Bi. Asma
Ramadhan Khamis akitoa shukrani mara baada ya uzinduzi wa Mradi huo.
Picha ya pamoja ya watendaji wa Wizara ya Afya wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Wizara hiyo
(wa kati kati) waliokaa Dkt. Jamala Adam Taib na viongozi wa Shirika la
Jhpiego baada ya uzinduzi wa miongozo ya Kitaifa ya kukinga na
kudhibiti kuenea kwa maambukizi ya magonjwa.(Picha na Makame Mshenga wa
Maelezo Zanzibar).
======= ========
NA RAMADHANI ALI/HABARI MAELEZO.
Wizara
ya Afya kwa kushirikiana na wahisani wa Maendeleo kutoka Marekani na
Shirika la Afya la Kimataifa la Jhpiego imezindua miongozo miwili ya
Kitaifa katika kukinga na kudhibiti kuenea kwa mambukizi ya magonjwa
katika Hospitali na sehemu za kutolea huduma za afya Zanzibar.
Miongozo
iliyozinduliwa ni wakuboresha viwango katika Hospitali na vituo vya
afya ili kuzuia na kudhibiti maambukizo na ule unaobainisha vigenzo
vya tathmini ili hospitali ziweze kutambuliwa na kupewa tunzo
zitakazobainisha jitihada za vituo katika kufikia viwango vya ubora vya
kitaifa.
Akizindua
miongozo hiyo katika sherehe zilizofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja,
Kaimu Mkurugenzi Wizara ya Afya Dkt. Jmala Adam Taib amewataka madaktari
na wafanyakazi wa vituo vya afya kubadilika katika kutoa huduma ili
kupunguza maabukizi ya magonjwa wakati wa kutoa huduma kwa wagonjwa.
“Imebainika
kati ya wagonjwa 100 wanaofikishwa katika Hospitali na vituo vya afya
Unguja na Pemba, 15 kati yao wanapata magonjwa mengine mapya wakiwa
sehemu hizo jambo ambalo linaongeza gharama za matibabu kwa wagonjwa
hao,”alisema Dkt. Jamala.
Ameshauri
kuanzisha utaratibu utakaohakikisha maeneo ya kutolea huduma za
afya zinakinga na kudhibiti kiwango cha maambukizi ya magonjwa ili
kuwalinda wananchi na kuhakikisha wananchi wanapata huduma salama na za
kiwango cha juu.
“Miongozo
hii isaidie kuzifanya Hospitali zetu ziwe sehemu za wagonjwa kwenda
kupata huduma na sio kuishia kupata maambukizi mapya na kuwaongezea
mzigo na madhara zaidi,” alisisitiza kaimu Mkurugenzi Wizara ya Afya.
Amesema
kitu muhimu kwa wafanyakazi ni kushirikiana katika kuzitunza na
kuziendeleza nyenzo zilizopo katika Hospitali na vituo vya afya na
kuzifanyia matengenezo ambazo haziko katika hali nzuri ili kufikia lengo
lililokusudiwa.
Dkt.
Jamala ameongeza kuwa miongozo hiyo pia itasaidia kuwalinda watoa
huduma na jamii nzima katika hatari ya kupata maambukizo wakati
wakiwasaidia wagonjwa.
Akizungumza
katika hafla hiyo Mkurugenzi wa Mradi wa kudhibiti na kuzuia maambukizo
ya magonjwa unaosimamiwa na Shirika la Jhpiego Dkt. Albert Komba
ameahidi Shirika hilo litaendelea kushirikiana na Wizara ya Afya ili
kuhakikisha kiwango cha maambukizo mahospitalini kinapungua.
Amewashauri
wataalamu wa Afya na wafanyakazi wa Hospitali na vituo vya
Afya kutekeleza wajibu wao na kuunga mkono mpango huo kwa vitendo na
Shirika la Jhpiego litaendelea kuwajengea uwezo ili uweze kufanikiwa.
Dkt.
Albert amesema Hospitali na vituo vya Afya vya Tanzania Bara
vilivyoanzisha mpango huo zimepata mafanikio makubwa na ameeleza
matumaini yake kwamba Zanzibar itanufaiki zaidi katika mpango huo.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment