UK yakumbwa na uhaba wa mbegu za kiume
Uingereza
inakabiliwa na upungufu wa Mbegu za kiume hali ambayo huenda ikalazimu
kiliniki za matibabu ya uzazi nchini humo kuchukua mbegu duni.
Onyo hili limetolewa na shirika la kijamii la matibabu ya uzazi nchini humo BFS.
Inadaiwa kuwa baadhi ya kliniki hizo hutegemea shahawa kutoka nchi za kigeni kutokana na mahitaji yake nchini humo.
Lakini
mwenyekiti wa shirika hilo Daktari Allan Pacey amesema kuwa ana
wasiwasi kwamba baadhi ya vituo hivyo vya matibabu sasa vinatumia kila
njia ili kupata wafadhili wa mbegu hizo.
Amesema kuwa wanawake watakabiliwa na mbinu zitakazogharimu kiasi kikubwa cha fedha iwapo mbegu duni zitatumiwa.
Inadaiwa
kuwa upungufu huo unasababishwa na kuondelewa kwa sheria kwamba majina
ya wanaotoa mbegu hizo sasa ni sharti yajulikane ikilinganishwa hapo
awali ambapo watu wengi walipendelea kuficha majina yao.
Mahitaji
ya wafadhili wa shahawa yanazidi kushuka kwa kuwa maendeleo ya matibabu
ya uzazi yanawafanya wanaume wengi kutafuta watoto wao wenyewe.
Hatahivyo uhaba wa wafadhili wa mbegu za kiume bado upo.
Takwimu
kutoka mamlaka ya kudhibti uzazi wa binaadamu zinaonyesha kuwa moja
kati ya mbegu nne za kiume zimetoka katika mataifa ya kigeni.
Takwimu hizo zilikuwa moja katika kila mbegu kumi mnamo mwaka 2005.Chanzo BBC Swahili
No comments:
Post a Comment