Header Ads

SSEBO AJIUNGA EFM




Dennis Busulwa a.k.a Ssebo.
Mtangazaji maarufu nchini wa vipindi vya Radio na Television Dennis Busulwa a.k.a Ssebo amejiunga na Radio ya Efm ambayo imekwishajizolea umaarufu mkubwa jijini Dsm kwa kipindi kifupi tu kutokana na staili yake tofauti ya urushaji matangazo nchini.
Ssebo mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka mitano kwenye vituo mbalimbali vya Radio na TV amejizolea sifa na mashabiki lukuki katika tasnia hii ya utangazaji kutokana na staili na vituko vyake awapo hewani. 
"Mashabiki wangu watarajie mengi mazuri kutoka kwangu nikiwa na EFM", alisema Ssebo. Ssebo anakutana na timu ya watangazaji wengine wakongwe kama Dj Majey, Dizzo One na Sos B waliokwisha anza kusikika Redioni hapo.

No comments:

Powered by Blogger.