SIKO SELI YAKATISHA UHAI WA MEMBA WA CALI SWAG DISTRICT
kundi
la muziki wa Hip Hop toka nchini Marekani ‘California Swag District’
limepatwa na pigo jingine la kumpoteza mwanachama mwenzao anayefahamika
kwa jina la Cahron Childs AKA ”Jayare” aliyekuwa akisumbuliwa na
ugonjwa wa siko seli kwa kipindi kirefu.
Kwa mujibu wa tovuti ya MTV iliandika kwamba Jay alikuwa
akisumbuliwa na ugonjwa wa Siko Seli Anemia na alilazwa hospitalini
Alhamisi pasipo na sababu maalum na masaa machache baadaye mapigo yake
ya moyo yalisimama na kufariki Dunia.
Wakali hao waliowahi kusumbua na ngoma yao ya ‘Teach Me How To Dawg’ huku vichwa kama vile C-Smoove, Yung, M-Bone na Cahron “JayAre” wakiunda kundi hilo.
“Siko Seli imechukua uhai wa kaka yangu leo.” aliandika General
Da Smoove ambaye ni memba wa kundi hilo kwenye ukurasa wake wa Twitter
akionyesha kuhuzunishwa, haikuishi hapo mkali mwingine wa CSD aitwaye
Smoove nae pia aliandika kwenye mtandao wa Twitter “With
that being said I’m proud to know that with that disease he made the
best of his life … I jus(sp) saw my bro literally fight for his life I
told him ‘I love you bro’ hope’n he heard me.”
Cha kusikitisha zaidi, Jay sio mwanafamilia wa kwanza wa
Cali Swag District kupoteza maisha kwani inakumbukwa kuwa mwaka 2011
aliyekuwa memba wa kundi hilo M-Bone aliuwawa baada ya kushambuliwa na
risasi na watu wasiojulikana waliokuwa kwenye gari huku uhasama na
mabifu ya mtaani yakitajwa kuwa chanzo.. RIP JayAre.
No comments:
Post a Comment