Rais Kikwete aapisha Balozi na Wajumbe wa Tume ya Operesheni Tokomeza
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amemwapisha balozi mmoja pamoja na wajumbe wanne wa Tume ya Operesheni Tokomeza katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.Balozi aliyeapishwa ni Joseph Edward Sokoine ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.Wajumbe walioapishwa nia pamoja na Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Mstaafu Hamisi Amiri Msumi,Jaji Mstaafu Steven Ernest Ihema,Jaji Mstaafu Vincent Damian Lyimo pamoja na katibu wa tume hiyo Bwana Frederick Kapela.
Balozi Joseph Edward Sokoine akupokea miongozo ya kazi na kupongezwa na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
Balozi Joseph Edward Sokoine akipongezwa na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete. Wajumbe wa Tume ya operesheni Tokomeza wakiwakatika picha ya pamoja na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal(Wanne Kushoto) na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(Wapili kulia) wajumbe hao kutoka kushoto ni Katibu wa Tume hiyo Bwana Frederick Kapela Manyanda, Jaji Mstaafu Vincent Damian Lyimo(wapili kushoto), Jaji mstaafu Hamisi Amiri Msumi(Watatu kushoto), na Jaji Mstaafu Steven Ernest Ihema(kulia),Wasita kushoto ni Balozi Joseph Edward Sokoine(picha na Freddy Maro)
No comments:
Post a Comment