Header Ads

Picha na Taarifa Kutoka Gazeti la Mwananchi LEO:Mtoto Nasra Rashid Mvungi (4), aliyefichwa kwenye boksi kwa miaka minne, amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na katika saa zake za mwisho za uhai wake alisikika akitamka maneno “sitaki waje kunichukua”.


Mtoto aliyekuwa amefichwa kwenye boksi kwa miaka mitatu mfululizo Morogoro,Nasra Rashid (4),akiwa kwenye Wodi B ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH)alikohamishiwa kwa matibabu zaidi. Picha na Beatrice Moses.  
---
 Mtoto Nasra Rashid Mvungi (4), aliyefichwa kwenye boksi kwa miaka minne, amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na katika saa zake za mwisho za uhai wake alisikika akitamka maneno “sitaki waje kunichukua”.

Nasra ambaye alikuwa akitibiwa MNH, alifariki dunia usiku wa kuamkia jana baada ya hali yake kubadilika Alhamisi iliyopita, kiasi cha kuhamishiwa katika chumba cha uangalizi maalumu (ICU) ambako aliwekewa mashine ya kumsaidia kupata hewa ya oksijeni.
Mama mlezi wa Nasra, Josephine Joel alisema kabla hajawa mahututi, mtoto huyo alikuwa akiweweseka kwa kuzungumza maneno mengi hali iliyosababisha wauguzi kumfanyia ibada maalumu.

No comments:

Powered by Blogger.