PICHA KUTOKA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI WIZARA YA MAMBO YA NCHI:NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA MABANDA MAONYESHO UTUMISHI WA UMMA DAR
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mwamini Malemi (kushoto) akiondoka katika Viwanja vya Mnazi Mmoja baada
ya kumaliza kuangalia na kujifunza zaidi shughuli mbalimbali zinazofanywa
na Wizara yake katika maonyesho hayo yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
(Nida), Dickson Maimu akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu, Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (wapili kulia) katika Banda
la Nida kujifunza masuala mbalimbali ya kiutendaji yanayofanywa na Mamlaka
hiyo iliyopo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika Maonyesho ya Wiki
ya Utumishi wa Umma yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa
Habari wa Wizara hiyo, Christina Mwangosi.
Koplo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Loyce Abeid, akimuonyesha Naibu Katibu Mkuu, Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kushoto) kifaa kinachotumika
kwa ajili ya uokozi wa magari yanapopata ajalia hasa magari ya tenki.
Malemi alitetembelea Banda la Wizara na Taasisi zake katika Maonyesho
ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja,
jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi
(kushoto) akimuuliza maswali Afisa wa Idara ya Uhamiaji, Mathew Ikomba
kuhusu matatizo mbalimbali likiwemo baadhi ya wananchi wanailalamikia
Idara hiyo kuhusu uombwaji wa rushwa wakati wanapoomba kupatiwa Hati
ya Kusafiria (pasipoti). Malemi aliitaka idara hiyo ifuate haki wakati
wananchi wanapoomba pasipoti. Wizara na Idara zake inashiriki katika
Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya
Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment