PICHA KUTOKA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI:TASWIRA ZA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI MATHIAS CHIKAWE, IGP NA KAMISHNA MKUU UHAMIAJI WAKIWA ZIARANI CHINA
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kushoto), Inspekta
Jenerali wa Polisi (IGP)
Ernest Mangu (kushoto), Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylvester
Ambokile (wanne kushoto) wakipokea taarifa kuhusu Mfumo wa Ufuatiliaji
wa Mienendo ya Watu (Public Surveilance Sytem (Global eye) kutoka kwa
Mtaalam wa Kampuni ya Telecom ya nchini China. Waziri Chikawe na ujumbe
wake wapo jijini Beijing, China kwa ziara ya kikazi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto)
akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Kampuni ya Kutoa Huduma ya
Mawasiliano
nchini China, Li Ping alipokuwa akimfafanulia masuala mbalimbali ya
mawasiliano yanayofanywa na Kampuni yake. Waziri Chikawe yupo jijini
Beijing nchini humo na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu,
Kamishna Mkuu wa Idara
ya Uhamiaji, Sylvester Ambokile kwa ajili ya ziara ya kikazi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe
(wapili kushoto), Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu,
Kamishna
Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylvester Ambokile wakiwa katika picha ya
pamoja na Mwenyekiti wa Kampuni ya Kutoa Huduma ya Mawasiliano nchini
China, Li Ping. Waziri Chikawe na ujumbe wake wapo jijini Beijing, China
kwa ziara ya kikazi. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment