Header Ads

JUMA PINTO MGENI RASMI KATIKA BONANZA LA TASWA ARUSHA

  picha ikionyesha katibu wa chama cha waandishi wa habari  Mussa Juma  akiwa  na mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari za michezo, Arusha (TASWA) Jamila Omary wakiwa wana pokea cheki ya  shilingi   milioni moja na laki tano  kutoka kwa meneja masoko wa  Megatrade  Gudluck Kwayu katika ukumbi wa hoteli ya palace mkoani Arusha.

katibu wa taswa wa kwanza  kushoto  Musa juma akiwa anaongea na waandishi wa habari kuhusiana na bonanza la taswa linalotarajiwa kufanyika jumamosi katika viwanja vya general trye jijini hapa wa katikati ni meneja matukio wa TBL Chris Salakana (picha zote na woinde shizza,Arusha.

Na Woinde Shizza,Arusha

 Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari za michezo nchini
(TASWA), Juma Pinto, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika bonanza la
vyombo vya habari kanda ya kaskazini, June 28 mwaka huu ambalo
limedhaminiwa na kampuni ya hia nchini (tbl)

Katibu wa TASWA mkoa wa Arusha, Mussa Juma akizungumza na waandishi wa   habari, palace hoteli katika kikao cha kutangaza zawadi na wadhamini wa bonanza hilo.alisema maandalizi ya bonanza hilo  ambalo wadhami  wakuu ni kampuni ya bia nchini (TBL) yamekamilika.



Alisema Pinto ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya  hifadhi ya Mamlaka ya
Ngorongoro, anatajiwa kutoa zawadi kwa washindi, ambapo bingwa anavuna    kikombe na fedha taslimi 200, 000.



Mshindi wa pili katika soka atavuna 100,000, mshindi mpira wa pete
atavuna 100,000 huku timu yenye nidhamu itapokea tsh 50, 000.

Awali Mwenyekiti wa Taswa mkoa wa Arusha, Jamila Omar alisema timu za   wanahabari na wadau wa habari, watachuana katika soka, mpira ya pete,  kuvuta kamba, kukimbiza kuku, mbio za magunia.



Aliwataja wadhamini wengine kuwa ni Mega trade, Mamlaka ya hifadhi
Ngorongoro, Kampuni ya Tanzanite forever,  TANAPA,Coca Cola, Pepsi
Arusha, Aicc na palace Hotel.

Timu ambazo zitashiriki ni Triple A, Sunrise radio, AJTC, Wazee Klabu,
Taswa Arusha, Radio 5, ,Arusha One, Mj radio, Radio ORS kutoka mkoa wa
Manyara na  NSSF.

Katika kikao hicho, ,Meneja masoko wa mega Trade alikabidhi the hundi
ya udhamini kiasi cha Tsh 1.5 milioni huku, Meneja matukio wa TBL
kanda kaskazini  Fred Sarakana akitangaza Tbl kuendelea kuwa wadhamini   wakuu wa bonanza hilo na kuwataka wanahabari kujitokeza kushiriki.

No comments:

Powered by Blogger.