Exim FC yaichapa PWC 5-2 mechi ya kirafiki
Kiungo wa timu ya Exim Bank FC,Mustafa Juma (kulia)
akikokota mpira wakati wa mechi ya kirafiki na timu ya PWC iliyochezwa
katika uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Exim
Bank FC ilishinda kwa magoli 5 – 2.
Mchezaji wa timu ya Exim Bank FC,Edwin Setebe akikokota
mpira wakati wa mechi ya kirafiki na timu ya PWC iliyochezwa katika
uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Exim Bank FC
ilishinda kwa magoli 5 – 2.
TIMU ya Benki ya Exim maarufu kama 'Innovation Team’ imeichapa PWC mabao 5 - 2 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Wakati
wa mechi hiyo iliyoshuhudiwa na watazamaji mbali mbali, timu ya Exim FC
iliyoongoza kwa upande wa umilikaji mpira na kuweza kujipatia goli la
kwanza katika dakika ya 20 shukrani zikimwendea mchezaji Lusajo
Adam, wakati katika dakika 22 kiungo Norbert Misana aliipatia timu hiyo
goli la pili, mpaka kipindi cha kwanza kinaisha Exim FC ilikuwa
ikiongoza kwa goli 2-0.
PWC
walifanya mabadiliko katika kipindi cha pili yaliyowaletea matunda na
kuweza kupata magoli katika dakika ya 47 na 54 ya mchezo baada ya
kupata nafasi mbili za wazi kutokana mabeki wa timu ya Exim FC kushindwa
kuwazuia washambuliaji wa PWC kuto funga magoli ya kusawazisha.
Exim
FC kupitia mchezaji Norbert Misana aliweza kufunga mabao mengine
mawili, goli la tatu likifungwa katika dakika ya 55 na goli la nne
likipachikwa kimyani katika dakika ya 70 ya mchezo kabla ya Rogers
Timoth kumalizia karamu ya mabao katika dakika ya 85 lililowawezesha
Exim FC kuibuka na ushindi baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa.
Akizungumza
muda mfupi baada ya kipenga cha mwisho cha mchezo kupulizwa, Norbert
Misana ambaye aliibuka mchezaji bora wa mechi hiyo alisema mechi hiyo
ilikuwa rahisi zaidi ikilinganishwa na mechi zao nyingine zilizopita.
"Tumecheza mchezo mzuri zaidi ukilinganisha na mpinzani wetu. Leo
timu yetu ilikuwa imejipanga vizuri zaidi hususani katika nafasi ya
katikati, na ndiyo maana tuliweza kuudhibiti mchezo kapita vipindi
vyote. Tumeweza kucheza kitimu katika muda wote wa mchezo kitu ambacho kimetusaidia tuweze kutengeneza nafasi nyingi za magoli.
"Wapinzani wetu, PWC ni timu bora, lakini leo nadhani timu yetu, kila mchezaji amekuwa katika fomu kutokana na mazoezi ya kutosha tuliyokuwanayo na tunaamini tukiendelea na hali hii, timu yetu itafika mbali kimchezo.
"Tumekuwa
tukifanya mazoezi kila mwishoni mwa wiki. Hali hii ya mazoezi kwa wiki
sio tu inatujenga kiuwezo ili kumfunga kila tunaekutana nae lakini pia
yanatuweka imara kiafya na kiakili na hivyo kuweza kutekeleza majukumu
yetu vizuri na kwa ufanisi kama wafanyakazi wa Benki ya Exim,” alisema
Norbert Misana.
No comments:
Post a Comment