Wazazi
wa mtoto Adorotea miezi mitatu iliyopita wakiwa uwanja wa ndege mbeya
wakisubiria ndege kuelekea DSM kwa upasuaji wa mtoto huyo.
Mtoto
Adorotea Emmanuel Njavike mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu aliyekuwa
anakabiliwa na majeraha ya moto na kusababisha ulemavu wa shingo
amafanyiwa upasuaji katika Hospitali ya CCBRT iliyoko Dar es Salaam na
sasa hali yake inaendelea vema.
Mama
mzazi wa mtoto huyo Milika Kaberege(35) alisema kuwa mwanawe alipata
majeraha hayo baada kuangukia motoni mwezi Octoba mwaka jana wilayani
Njombe na kupatiwa matibabu Mbeya bila mafanikio.
Baada
ya kuendelea kukosa matibabu yakinifu ndipoalionwa na vyombo mbalimbali
vya habari na habari zake kuandikwa ndipo Bohari ya Madawa nchini MSD
walipojitokeza kutoa usafiri wa ndege kutoka Mbeya kwa kushirikiana na
Kikundi cha Wanawake ambaio walimfikisha CCBRT mwezi Machi mwaka huu.
Milika
alisema kutokana na juhudi kubwa za Madaktari wa Hospitali hiyo mwanawe
amefanyiwa upasuaji mara mbili na kwamba hali yake inaendelea vema na
bado juhudi za Madaktari hao zinaendelea kurekebisha viungo vya mwanawe
ikiwa ni pamoja na mikono yote miwili ilyopata majeraha.
Mama
huyo ameshukuru Asasi mbalimbali zilizohangaikia matibabu ya mtoto wake
wakiwemo waandishi wa habari wa Mbeya yetu ambao wamefuatilia maendeleo
ya mtoto hata kufika Wodini kumjulia hali hivi karibuni na ameendelea
kupata Faraja siku hadi siku kutoka kwa wadau wanaofika Hospitali.
Aidha
amesema huenda mwanawe akatoka hivi karibuni baada ya kufanyiwa
upasuaji wa mwisho wa mikono na haamini kwamba mwannae ambaya alikuwa
akipata shida hata kula chakula na sasa anaweza kula na kutokana na
juhudi kubwa za madaktari mtoto wake hivi sasa ameanza kutembea.
Mama
Milika ametoa wito kwa wazazi na walezi wenye watoto wenye ulemavu
kuacha kuwaficha ndani bali wawapeleke Hospitali kama ya CCBRT ambao
wanafanya kazi ngumu ya kurekebisha viungo na wagonjwa kurejea katika
hali ya kawaida kutoa wito kwa wagonjwa kutokata tamaaa hali.
Upasuaji
wa awali wa Adorotea ulifanyika Machi 21 mwaka huu wakati ule wa pili
ulifanyika Mei 16 mwaka huu na upasuaji wa tatu utafanyika wakati wowote
kuanzia sasa na kuruhusiwa kurudi nyumbani.
Kwa yeyote anayeguswa kutoa msaada wa hali na mali anaweza kumpatia kupitia simu yake ya mkononi namba 0753913472.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment