HALMASHAURI ZATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO MIRADI YA MAENDELEO
Mkurugenzi Mkuu
wa wakala wa barabara (TANROADS) ,Injinia Patrick Mfugale akizungumza
katika uzinduzi wa mradi wa Arusha-Holili /TAVETA –VOI kilometa 122
pamoja na Arusha –bypass (km 42) unaofadhiliwa na benki ya maendeleo ya
Afrika (ADB)uliyofanyika jijini Arusha
======= =======
Aidha
kumekuwepo na changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikikwamisha miradi
hiyo ikiwemo ya wananchi kukataa kulipwa fidia kwa taratibu za sheria
za nchi ili kutoa maeneo ya kuchimbwa changarawe, kokoto na kuchota
maji.
Hayo
yalisemwa juzi na Mkurugenzi Mkuu wa wakala wa barabara (TANROADS)
,Injinia Patrick Mfugale wakati akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa
Arusha-Holili /TAVETA –VOI kilometa 122 pamoja na Arusha –bypass (km
42) unaofadhiliwa na benki ya maendeleo ya Afrika (ADB) uliofanyika
katika ukumbi wa naura springs mjini hapa.
Alisema
kuwa,kumekuwepo na changamoto kubwa sana zinazosababishwa na wananchi
na baadhi za halmashauri katika utekelezaji wa miradi hiyo hali ambayo
imekuwa ni kikwazo kikubwa katika kufikia malengo yaliyowekwa.
Alifafanua kuwa,
halmashauri za wilaya pamoja na serikali za vijiji wamekuwa wakitoza
kodi mbalimbali kwa vifaa vya ujenzi kama kifusi, mchanga,kokoto,na
maji.
Mfugale
alisema kuwa,mradi wa ujenzi wa barabara ya Arusha-holili ni sehemu ya
mradi wa kimataifa unaojulikana kwa jina la Holili/Taveta –Voi
unaounganisha nchi yetu na nchi jirani ya Kenya utagharimu kiasi cha
dola za kimarekani milioni 223.
Alisema
kuwa, awamu ya kwanza ni kuijenga kwa njia nne sehemu ya barabara
kutoka Sakina –Tengeru (km 14.1) na Arusha bypass (km 42) kwa fedha za
mkopo kutoka ADB .
Aliongeza
kuwa, sehemu ya pili ni kuendeleza ujenzi wa njia nne kutoka Tengeru
hadi Usa river (km 8.2) na ukarabati wa sehemu ya barabara iliyobaki
hadi Holili baada ya kupata fedha.
Naye
Mwakilishi wa benki ya maendeleo ya Afrika (ADB), Injinia Patrick
Musa alisema kuwa kumekuwepo na changamoto kubwa ya hali ya hewa ambayo
imekuwa ikichangia mradi kukamilika kwa wakati na ucheleweshaji wa
ulipwaji wa fedha za wakandarasi .
Alisema
kuwa, wao kama benki ya maendeleo ya Afrika wataendelea kutafuta hela
kwa ajili ya maendeleo kwani ni fursa nzuri wao kushirikiana na serikali
ya Tanzania katika kuleta maendeleo.(jamiiblog Pamela Mollel)
No comments:
Post a Comment