HAWA NDIO WACHEZAJI 32 WANAOTARAJIWA KUNG'ARA ZAIDI NA KUONGOZA TIMU ZAO WAKATI WA FIFA WORLD CUP 2014
Fainali za Kombe la Dunia ni uwanja mpana. Ni mahali ambapo vipaji
na vipaji vya wanasoka duniani huonekana. Madalali wa kuvumbua na
kununua wachezaji [scouts] hufurika kwenye mashindano kama haya wakijua
wazi kabisa kwamba pale ndipo watakapoona “lulu” kwa ajili ya vilabu
vyao. Kwa maana hiyo kuna kila aina ya harakati za kimichezo na
kuonyesha na kuonyeshana vipaji. Hii sio kumaanisha kwamba wachezaji
wote mahiri hapa duniani walicheza katika fainali za Kombe la Dunia.La.
Wapo wasakata kabumbu kadhaa ambao hawakuwahi kugusa fainali hizi.Mfano
ni George Opong Weah na watu kama kina George West nk.
Lakini wakati wengine wakionyesha vipaji ili wang’amuliwe na
kubadilisha maisha yao ya kisoka,wapo wale ambao wanashuka dimbani
tayari wakiwa na majina [superstars] na ambao dunia tayari inakuwa
ikiwaangalia kwa makini kutaka kujua na kuona kile watakachokifanya.
Kila timu huwa na mchezaji ambaye hutizamwa zaidi. Kwa umombo unaweza
kumuita Key Player. Kila timu,kwa kupenda au kutopenda,huwa ina star
player. Hii haimanishi kwamba katika timu hakuna wachezaji wengine wenye
majina au wanaoweza pia kuwa stars.La. Ni sheria ya mmoja mmoja
inayozingatiwa hapa.
Kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali wa soka,wachezaji hawa 32
[mmoja kutoka katika kila timu inayoshiriki fainali za Kombe la Dunia
mwaka huu] ndio watarajiwa kuchomoza zaidi huko Brazil. Mpangilio huu
hapa ni kutokana na makundi ya FIFA World Cup 2014. NB: Orodha hii
inaweza kubadilika kwani imeandikwa kabla timu zote hazijathibitisha
wachezaji wake 23 iliyowachagua mwisho. Wengine wanaweza kuumia katika
siku hizi za mwisho na hivyo kutokwenda Brazil.Zingatia.
Hakuna ubishi kwamba Neymar anayechezea soka la kulipwa Barcelona
nchini Spain ndio gumzo kubwa kwa timu ya Brazil. Anatarajiwa kuongoza
mashambulizi ya The Kings Of Samba[Brazil]
Ingawa wachezaji wengine wa Mexico kama Chicharito na Giovani dos
Santos wanatajwa kama ma-star,Oribe Peralta ambaye anacheza katika ligi
ya nyumbani katika club ya Santos Laguna, ndiye anaaminika hivi sasa
kuwa star zaidi
Hakuna shaka kwamba Luka Modric ndiye mchezaji star zaidi hivi
sasa katika timu ya Croatia. Kiungo huyu ambaye hivi sasa anachezea timu
ya Real Madrid nchini Spain ameonekana wazi kuwa tegemeo sio tu katika
club bali nchi yake Croatia.
Ingawa ungetegemea mchezaji kama Samuel E’too kuendelea kuwa star
na tegemeo zaidi katika timu ya Cameroon, golikipa Charles Itandje ndio
tegemeo na ambaye wengi watapenda kumuona akiokoa mikwaji. Charles
ambaye anachezea timu ya Konyaspor nchini Uturuki[kwa mkopo kutoka PAOK
FC ya Ugiriki] aling’ara vilivyo katika mchezo dhidi ya Tunisia wakati
wa kuwania nafasi ya kwenda Brazil.Google utaona alichofanya.
Ingawa bado kuna utata kuhusu hali yake na kama atakuwa fit kabla
ya kuanza kwa fainali za Kombe la Dunia huko Brazil,Diego Costa
mshambuliaji mahiri wa timu ya Atletico Madrid anatarajiwa kuwa nyota wa
Spain. Lakini pia huenda akawa ndiye mchezaji atakayezomewa zaidi huko
Brazil kwani Diego ni mzaliwa wa Brazil na angeweza kabisa kuchezea
Brazil mwaka huu kama asingeamua kuchezea Spain[pia ni raia wa
Spain].Wabrazil hawajaipenda hiyo.
Robben,mshambuliaji mahiri ambaye hivi sasa anaendelea kuwika na
timu ya Bayern Munich nchini Ujerumani,ndiye mchezaji ambaye ni star
zaidi na ambaye ameonyesha kuwa na kile kiwango kinachoitwa “cha dunia”.
Ana miaka 30 hivi sasa.
HABARI ZAIDI BOFYA LINK HIYO HAPO
No comments:
Post a Comment