Raia wa Misri wanamchagua Rais mpya
Mabango yanayotangaza uwaniaji wa aliyekuwa Mkuu wa jeshi la Misri, Abdel Fatah al-Sisi, kama Rais
Raia
wa Misri wanapiga kura kwa muda wa siku mbili kumchagua rais mpya chini
ya ulinzi mkali kuhakikisha mchakato wa upigaji kura unafanyika kwa
usalama.
Karibu
maafisa wa usalama laki mbili wameshika doria kote nchini Misri
serikali ikionya dhidi ya hatari za usalama zinazoweza kusababishwa na
itikadi kali za kiislam .
Adbel
Fatah al-Sisi Kiongozi wa kijeshi wa zamani aliyeongoza mapinduzi ya
kijeshi dhidi ya rais wa awali Mohammed Morsi anatarajiwa kupata ushindi
kwa u rahisi.
Oparesheni
kubwa ya usalama inayoendelea nchini Misri ni ushahidi kamili kuwa
utawala wa sasa unaoungwa mkono na jeshi unatambua kuwa ugaidi unaoungwa
mkono na Waislamu wenye itikadi kali upo na unaweza kuteguliwa wakati
wo wote.
Mbinu
ya kukabiliana na ugaidi huo ya Abdel Fatah al-Sisi haijabadilika ila tu
ni magwanda yake ya kijeshi ya field Mashel yaliyojaa medali
yaliyobadilishwa na nguo za kiraia.
Ametangaza
katika kampeni yake kuwa anaunga mkono kuangamizwa kabisa kwa kundi la
Muslim Brotherhood ambalo limeshuhudia maelfu ya wanachama wake
wakizuiliwa na mamia wakihukumiwa vifo.
Bwana
Sisi ametoa wito kwa watu wanaotakia Misri amani na utangamano baada ya
miaka kadhaa ya mapinduzi na ghasia na ameheshimiwa kiwango cha
kusujudiwa na wengine hivi kwamba unaweza kununua peremende au chokoleti
dukani iliyopachikwa picha yake.
Mpinzani
wake mwenye mrengo wa kushoto, Hamdeen Sabbahi, anatajwa katika vyombo
vya habari ambavyo vinaoenekana kuamua tayari kuwa yeye atashindwa
katika Uchaguzi unaoanza leo.
Ingawa
wapiga kura wana mazoea ya kubadilika dakika za mwisho kabla ya
uchaguzi lakini wengi nchini Misri watashangaa iwapo Bwana Sisi hashindi
uchaguzi huu, na tena kwa urahisi.Chanzo BBC Swahili
No comments:
Post a Comment