Header Ads

PICHA KUTOKA OFISI YA MAKAMU WA RAIS-IKULU:CHUNGU NA VIBUYU VILIVYOCHANGANYA UDONGO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR HADHARANI, DKT. BILAL ATEMBELE MAONYESHO YA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO JIJINI DAR ES SALAAM



  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu Chungu na Vibuyu, vilivyotumika kuchanganya Udongo wa Tanganyika na Zanzibar, mwaka 1964, kutoka kwa Mawazo Ramadhan wa Makumbusho ya Taifa, wakati alipotembelea kwenye Banda la Idara ya Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais, alipotembelea maonyesho ya Sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa na Ofisa wa Idara ya Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais, Martha Mashuki, baadhi ya Magazeti  yaliyochapishwa mwaka 1964, wakati alipotembelea kwenye Banda la Idara ya Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais, alipotembelea maonyesho ya Sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

No comments:

Powered by Blogger.