Mkapa atembelea shule ya msingi Manyara Ranchi,Wilayani Monduli
Rais
mstaafu wa awamu wa tatu Mh Benjamin Mkapa leo(jumatatu) amefanya ziara
kumtembelea Shule ya msingi ya Manyara Ranchi inayofadhiliwa na shirika
la kimataifa la uhifadhi wa wanyamapori la African wildlife foundation
wilayani Monduli.
Mzee
Mkapa ni Makamu mwenyekiti wa shirika hilo lenye makao yake mjini
Washington Marekani.picha mbalimbali zinamuonesha waziri mkuu mstaafu na
mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akimuongoza Rais Mkapa kuzuru shule
hiyo.
Rais
mstaafu wa awamu wa tatu,Mh. Benjamin Mkapa (katikati) akimsikiliza kwa
makini Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward
Lowassa wakati alipotembelea Shule ya msingi ya Manyara Ranchi
inayofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Wanyama pori la
African Wildlife Foundation,wilayani Monduli.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akimueleza jambo Rais mstaafu wa awamu wa tatu,Mh. Benjamin Mkapa wakati
walipokuwa kwenye moja ya madarasa ya shule hiyo.
Rais
mstaafu wa awamu wa tatu,Mh. Benjamin Mkapa akiagana na Waziri Mkuu
Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa.
No comments:
Post a Comment