RIDHIWANI KIKWETE AENDELEA KUZISAKA KURA JIMBO LA CHALINZE

Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete
akilakiwa na Wananchi wakazi wa Kijiji cha Chahua,Kata ya Bwilingu leo
Machi 27, 2014 wakati wa Muendelezo wa Kampeni zake za kuomba ridhaa kwa
Wananchi hao ya kuwa kiongozi wao kwa Maendeleo ya Jimbo la Chalinze.

Meneja
wa Kampeni za CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Steven
Kazidi akiwasisitiza Wananchi wa Kijiji cha Chahua kuzitunza vyema
Shahada zao za kupigia kura,ili siku ikifika ya kupiga kura wasipate
shida na waweze kupiga kura Mtu anaefaa kuwa Kiongoizi wa Jimbo la
Chalinze.


Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete
akiwahutubia na kutoa Sera zake kwa wananchi wa Kijiji cha Chahua,Kata
ya Bwilingu leo Machi 27, 2014 .

Mwenyekiti
wa Kijiji cha Chahua,Christina Kejeli (kulia) akitoa maelezo ya
Maendeleo ya Kijiji kwa Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la
Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kushoto) wakati wa
muendelezo wa Mikutano ya Kampeni iliyofanyika leo Machi 27, 2014
katika vijiji vya Chahua na Matuli,Kata ya Bwilingu.

Diwani
wa Kata ya Bwilingu,Ahmed Kalama akisisitiza jambo wakati wa
kuzungumzia mafanikio ya Kata yake pamoja na Changamoto ambazo bado
hazijafanyiwa kazi ndani ya Kata hiyo,mbele ya Mgombea Ubunge wa Jimbo
la Chalinze.

Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete
akiwasalimia wakina Mama wa jamii ya watu Wafugaji (Wamasai) wakati
alipowasili kwenye Kijiji cha Matuli kwa ajili ya kuendelea na Mikutano
ya Kampeni zake za kuomba ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze.Picha zote na Othman Michuzi.
No comments:
Post a Comment