Baraza la vyama vya siasa lataka wajumbe wa Bunge la Katiba kuweka mbele utaifa.
(Picha na Maelezo-Dodoma)
(Na Magreth Kinabo ,MAELEZO Dodoma)
KAMATI ya
Uongozi wa Baraza la Vyama vya Siasa inawaomba wajumbe wote wa Bunge
Maalum la Katiba kuzingatia kanuni kwani zinakataza vitendo vya utovu
wa nidhamu wakati wa vikao vya Bunge hilo .
Kauli
hiyo imetolewa leo mjini na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Peter
Mziray katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi
wa Bunge mjini Dodoma kufutia baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo kuonesha
vitendo visivyo na nidhamu ikiwemo kuzomea.
“
Kamati ya Uongozi wa Baraza la Vyama vya Siasa inawaasa wajumbe wote wa
Bunge Maalum la Katiba kubadilika na kuonesha nidamu ambayo Watanzania
wote wanategemea kutoka kwao,” alisema Mziray.
Alisema Kamati
hiyo inaamini kuwa mjumbe anaweza kutoa hoja yake nzito ya kukubali na
kupinga jambo ikakubalika au kukataliwa na wajumbe wengine wengine au
Mwenyekiti bila ya kuzomewa.
Aidha
Mwenyekiti huyo Mziray amemtaka Mwenyekiti wa Bunge Maalum kutoyatambua
makundi ya Tanzania Kwanza na UKAWA kwa kuwa sio makundi rasimu ndani
ya Bunge hilo na ndio yanasababisha vurugu kwa kuweka maslahi ya vya
siasa mbele badala ya Taifa.
Amewataka
wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kuacha kujihusisha na
makundi hayo badala yake wachambue na kuunga mkono hoja kwa uzito wa
hoja na kuzingatia masilahi ya taifa badala ya kuzingatia mtazamo wa
kundi fulani.
Mziray
ameongeza kuwa wajumbe wanatakiwa kuepuka vitendo ambavyo vinakwamisha
mchakato wa kupata Katiba mpya kwa mustakabali wa taifa hili na Wananchi
kwa ujumla.
Katika
hatua nyingine Mwenyekiti huyo amesema kuwa Kamati ya Uongozi imeona
ni vema wajumbe wa baraza hilo, wakuu wa vyama vya siasa, ambao si
wajumbe wa baraza hilo wakutane ili kujadiliana, kushauriana na
kuridhiana ili kuweza kufanikisha azma ya kupatikana kwa Katiba
Mpya kwa mwafaka.

No comments:
Post a Comment